Breaking News

Wanawake wameshauriwa kutupilia mbali urembo wa Kope.


Na Maridhia Ngemela, Mwanza


Hivi karibu kumekuwa na tabia ya baadhi ya wanawake kuweka urembo wa ubandikaji kope katika macho yao na kuchukulia ni kitu cha kawaida bila kufuatilia madhara ya upandikaji huo.



Dakitari wa magonjwa ya macho kutoka Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mwanza  Sokouture Elizabeth Makamba alipokuwa akizungumza na MPC blog ofisini kwake amesema kuwa ,wanawake wanaobandika kope wako hatarini kupata UPOFU.

Amefafanua kuwa, kope ni sehemu ya macho ambayo inapatikana kwenye kifuniko cha macho na kazii yake kubwa ni kumlinda jicho na kurekebisha mwanga unaoingia kwenye macho.

Ameongeza kuwa,changamoto kubwa ya wateja wake wanakuwa wameisha athirika na ubandikaji huo wa kope na kusababisha madhara ya macho yao.

Amesema kuwa macho ni kiungo laini sana ambacho hakiitaji kuchezewa ovyo ovyo hivyo kuweka kitu chochote kwenye jicho ambacho siyo kisafi kinaweza kusababisha kupata madhara makubwa ikiwemo kupoteza uwezo wa kuona.


Makamba amesema gundi zinazotumika kubandika hizo kope zinaweza kuleta aleji kwa mtumiaji kwa kupata muwasho,jicho kuvimba na hatimae kufanya macho yasione kutokana na ukosefu wa elimu kwa wapandikaji na wabandikwaji.


"Tabia ya ubandikaji wa kope bandia inaweza kuharibu mfumo mzima wa utengenezaji wa kope asili hali itakayopelekea uzalishaji wa kope kuwa mdogo na mwisho kujikuta hana kope kabisa kwasababu unapotumia ile gudi ni nzito na sii maalum kwa matumizi ya upandikaji kope unakuta mwingine anatumia hadi gundi ya superguluu kwahiyo ukija kuibandua inaondoka na zile kope asilia  ",amesema Makamba.


Kutokana na madhara hayo ambayo wanaweza kuyapata kwa kubandika kope Dk Makamba amewaasa watumiaji wa urembo huo  kuyapenda macho yao ili waweze kuyatunza.


"Pindi inapotokea umepata ugonjwa wa macho msipende kutumia dawa bila ushauri wa wataalamu wa afya ya macho,pia jengeni tabia ya kupima macho kila mwaka ili utakapogundulika na ugonjwa iwe rahisi kuanza tiba",amesema Makamba.


Kwa upande wake Prisca Pius ambae ni mfanyakazi wa saluni ya Paint Me iliyoko Jijini Mwanza amesema kuwa kuna aina mbili za ubandika wa kope machoni ambazo ni Kope ya mkanda na kope ya moja moja ambazo zote wateja wake hutumia kwaajili ya urembo.


Akifafanua aina hizo amesema kope ya mkanda haina madhara makubwa kutokana na aina ya kope hiyo kubandikwa bila gundi, lakini kope ya moja moja inamadhara kwasababu inatumia gundi ambapo wakati wa kubandua inaweza kutoka na kope za asili.


Pius amesema kuwa katika kipindi cha miaka tisa alichofanya kazi amekuwa na utatatibu wa kuwashauri wateja wake faida na hasara za uwekaji wa kope ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.

Nae kiongozi wa dini ya kiislam ambae ni imamu wa msikiti wa Ibadhi Mkoani Mwanza Nouh Mousa amesema kuwa dini imeruhusu mapamba kwa wanawake ili kuvutia kwa Waume zao.

Mousa amesema kuwa miongoni mwa mapamba yaliyokusudiwa ni upakaji Hina,wanja ,bangiri na cheni isipokuwa  mapamba ambayo sii asili ni haramu kwani unapotumia mapamba kama upandikaji kope tayali unakuwa umeisha mkosoa Mungu aliyekuumba.

No comments