Breaking News

DOTTO JAMES AWAFUNDA WAHITIMU VYUO VIKUU.

 Na Blandina Aristides. Mwanza.

Wahitimu wa vyuo vikuu na vyuo vya kati nchini wameshauriwa kutumia fursa zinazotolewa na taasisi za fedha Ili waweze kujiajili.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara,Dotto James ametoa rai hiyo  kwenye mahafali 14 ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Kampas ya Mwanza na mahafali ya 56 ya CBE  nchini.

Amesema kuwa kuna haja ya wahitimu kuandika maandiko biashara  na kuzitumia taasisi za fedha kwa ajili ya kupata mikopo ili kuweza kuanzisha miradi ambayo itawasaidia kujiajili na kuajili wenzao.

Amesema ili kuweza kufanikiwa ni lazima kuvaa uzalendo wenye heshima ili kupata taifa lenye maendeleo.


Kutokana na uhaba wa ajira nchi ni ni vema  wahitimu hao kuwa na maadili mema ili waweze kufikia malengo yao laikini pia kuwa wabunifu na wenye  kujishughulisha na shughuli mbalimbali.

“Lengo la serikali ni kuona chuo hiki kinaendelea kutoa elimu kwa wanafunzi ili waweze kupata elimu kama sera inavyotaka”,amesema Dk James.

Kwa upande wake  Mkuu wa chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Emmanuel Mjema amesema chuo kina mkakati wa  kuwaongezea uwezo wahitimu hao kwa kuwapa mipango ambayo itawasaidia wanafunzi kuanzisha biashara zao zitakazosaidia kujiajiri wenyewe.

“Tumeanzisha mpango mwingine wa mwanafunzi asome huku anafanya kazi tumeona wanafunzi wengi hawana ujuzi wa kufanya biashara kwani kupitia mikakati hii tutawasaidia ili waweze kujiajiri na kuajiri watu wengine kwani kufanya hivyo kutapelekea kunufaika na elimu wanayoipata kutoka chuoni hapo.

Prof.Mjema aliishukru Serikali kwa kununua eneo la chuo na majengo na kwamba chuo kitaendelea kufanya vizuri na kwamba , hakuna kitakachot warudisha nyuma na kushindwa kuwasaidia na kuwapa ujuzi wahitim ili waweze kutimiza ndoto zao za baadae,”

Prof.Wineasta Anderson ni  Mwenyekiti wa bodi ya uongozi wa chuo cha elimu ya Biashara amaye alieleza kuwa lengo kubwa la chuo ni kutoa wahitimu wanaojitambua katika tasinia mbalimbali ikiwemo ujasiliamali ili kutengeneza Taifa la watu wanaojitengemea.

Alisema pamoja na kutoa Elimu stahiki na yenye weledi kwa wanafunzi, bado Chuo kinakabiliwa na changamoto mbalimbali  huku akiiomba Serikali iweze kuzitatua kadili itakavyo wezekana.


Alizitaja changamoto hizo kua ni pamoja na miundombinu ya barabara,umeme,na bweni Moja la wanafunzi ambalo  linahitaji kufanyiwa ukarabati.

Jumla ya wahitimu 484 wametunukiwa Astashahada, Stashahada na Shahada wakiawemo wanaume 257 na wanawake 227.

No comments