Breaking News

Huduma za afya zazidi kuboreshwa Jijini Mwanza

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel akizungumza na wataalamu wa afya juu ya kuboresha huduma za afya kwa wamama wajawazito sanjari na kupunguza vifo vya Watoto wachanga.

Na Hellen Mtereko, Mwanza.

Wataalamu wa huduma za afya wamekutana leo hii mkoani Mwanza kwa lengo la kujadili mwenendo wa huduma za afya na vifo vya wazazi na watoto wachanga.

Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza  na kufunguliwa na Muhandisi Robert Gabriel ambae ni Mkuu wa Mkoa huo.


Amesema kuwa wataalamu hao waangalie ni nini chanzo cha vifo hivyo ilikuendelea kuokoa maisha ya mama na mtoto.

"Timu zenu zitembee kwenye nyumba za ibada ili tuweke hamasa ya ukusanyaji damu ambayo itasaidia zaidi kupunguza vifo hivyo naomba kila wiyala iweke hamasa ya kuchangia damu mfano Wilaya ya Misungwi wamefanya vizuri kwahiyo tuweke kampeni ili tupate damu ya kutosha tupunguze changamoto hizi na tuweze kurudisha uhai wa binadamu amesema Gabriel.


Muhandisi Robert ametoa maagizo kwa Wakuu wa Wilaya Mkoani hapa kuwa wa tengeneze mfumo wa kumfuatilia mama  mjamzito na  kujadili vifo vya akina mama kila mwezi ili kuona namna ya kumsaidia.

" katika kumfatilia mama mjamzito inatakiwa muhakikishe  afya yake inazidi kuwa imara kwa kuangalia  lishe, malaria , mwenendo wake wa mahudhurio ya kliniki na tuzidi kutoa elimu zaidi kila mara",

Mwishooo

1 comment:

  1. happyluke happyluke 바카라사이트 바카라사이트 1xbet 1xbet bet365 bet365 10cric login 10cric login 10cric 10cric 카지노 카지노 우리카지노 우리카지노 sbobet ทางเข้า sbobet ทางเข้า 413

    ReplyDelete