Breaking News

Kampuni ya Mysol imetoa msaada wa Sola katika Hosptali ya Mkoa wa Mwanza.

Na Hellen Mtereko, Mwanza

Kampuni ya Mysol imetoa msaada wa Sola yenye thamani ya sh, million 3.4 katika Hosptali ya Mkoa ya Sokouture itakayofunga wenye wodi ya wazazi  yenye ukubwa wa wati 200 na taa 20  kwaajili ya kuwa na mwanga wa uhakika pindi umeme unapokati.

Mkuu wa Wilaya ya Magu Sallum Kalli (Kushoto) akikabidhi Sola kwa muwakilishi wa hospital ya Sokouture leo hii Jijini Mwanza.

Msaada huo umetolewa Leo tarehe 12/02/2022 wakati wa uzinduzi wa jina jipya la kampuni hiyo iitwayo Mysol iliyotokana na muunganiko wa kampuni tatu ambazo ni  Mobisol, power corner na Finix.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi Sola kwa muwakilishi wa hospital ya Sokouture Mkuu wa Wilaya ya Magu  Mh Salum Kalli amesema kuwa kampuni ya Mysol imejipambanua katika kuhakikisha Jamii inapata huduma ya Umeme jua, hali inayosaidia shughuli mbalimbali kuendelea pindi umeme unapokuwa umekatika.


Kalli amesema mji wa Mwanza ni kitovu cha biashara  hivyo amezitaka Kampuni nyingine za umeme wa jua kuwekeza sanjari na kutoa ushirikiano kwenye Jamii kama walivyofanya  Mysol.

Kwaupande wake Meneja wa Kanda ya ziwa kutoka Kampuni ya Mysol Pinel John amesema kuwa wameona ni vyema watoe Sola hiyo katika wodi ya wazazi ili kupunguza changamoto ya kukosa mwanga kwa wazazi pindi umeme unapokatika au pale panapotokea hitilafu ya Umeme.

John amesema kuwa wanaendelea kutoa huduma hiyo ya umeme jua katika sehemu mbalimbali ili watu waondokane na matumizi ya mishumaa hali itakayoweza kupunguza majanga ya moto na kuwa na chanzo cha nishati cha uhakika.


No comments