Breaking News

MSEMAJI MKUU WA SERIKALI ATOA VYETI NA ZAWADI ZA PONGEZI KWA WAANDISHI WA HABARI WA MKOA WA MWANZA WALIOSHINDA TUZO ZA EJAT 2020

Na Tonny Alphonce,Mwanza.


Msemaji Mkuu wa serikali Bw Gerson Msigwa leo 17 Oct 2021, katika taarifa yake ya wiki ya serikali Aliyotoa katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Bw. Msigwa amepata  wasaha wa kupongeza juhudi za kina zinazofanywa Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa Habari wa Mwanza, Bw Edwin Soko kwa kuwaunganisha waandishi wa habari na kuwa wamoja katika kazi zao za kila siku.

Pia ametoa vyeti vya pongezi na zawadi mbalimbali Kwa waandishi wafuatao,Projestus Binamungu,Kisali Simba,James Lerombo na Regina Patrick ambao walioshinda Tuzo za EJAT 2020 katika vipengele tofauti tofauti.
Msigwa amewaasa waandishi kufanya kazi Kwa ajili ya maendeleo ya Taifa na kutoa taarifa Kwa klabu za waandishi wa habari na pia kuwasiliana na maafisa habari wa Mikoa endapo itatokea taharuki.

Msemaji Mkuu wa Serikali alipata nafasi ya kuulizwa maswali na waandishi ambapo Mwenyekiti wa MPC bwana Edwin Soko alitaka kujua juu ya utayari wa Serikali kwenye kutekeleza hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Haki ya Afrika ya Mashariki juu ya kufutwa kwa baadhi ya vipengele vya Sheria ya Huduma ya vyombo vya habari.

Akijibu swali hilo Bwana Msigwa alisema kuwa,anachojua baada ya hukumu hiyo Serikali ilikata rufaa na hivyo kwa sasa suala jambo hilo lipo chini ya taratibu za Mahakama likisubiri maamuzi.

Na kuhusu swali la pili la mwenyekiti Soko juu ya mwandishi Azory ambae hadi leo hakuna taarifa rasmi iliyotolewa hadi sasa kuhusiana na kifo chake,Msingwa alisema kuwa,suala la Gwanda lilo chini ya upelelezi wa Jeshi la Polisi na litakapokamilika taarifa itatoka.

Msigwa pia alizungumzia suala la utayari wa Serikali kwenye kuwalinda waandishi wa habari na kuwaahidi kuwa, Serikali ipo kazini kwenye kuhakikisha usalama wa Waandishi nchini na kuwataka kutoa taarifa kila wanapokuwa katika mazingira ya hatari ili waweze kusaidiwa.

katika mkutano huo wa taarifa ya wiki ya msemaji wa serikali Msigwa alizitambulisha picha rasimi za ukutani kwa upande wa Rais wa Jmuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na Makamu wa Rais Philp Mpango na kuwataka wananchi wanaohitaji picha hizo wahakikishe wanapata picha halisi alizozitambulisha

No comments