Breaking News

DESK & CHAIR FOUNDATION YAKABIDHI HUNDI KWA MPC

Na Mwandishi Wetu.

Mwenyekiti wa Mwanza Press Club Bw. Edwin Soko akipokea hundi ya laki 4 kutoka kwa Bw. Meghi ambae ni mwenyekiti wa Desk & Chair Foundation.

Taasisi ya The Desk & Chair Foundation imekabidhi hundi ya kiasi cha laki nne (400,000) kwa klabu ya Waandishiwa habari ya Mkoa wa Mwanza (MPC) ikiwa ni jitihada za kuchangia mfuko wa kusaidia wanachama wa MPC ( MPC solidarity Fund).

Akikabidhi hundi hiyo Mwenyekiti wa Desk & Chair Foundation Bwana Meghi amesema kuwa, ataendelea kutambua mchango unaofanywa na waandishi wa habari wa Mkoa wa Mwanza.

Bwana Meghi amewapongeza MPC kwa kuanzisha mfuko huo na kuwataka wanachama hao kuhakikisha wanauchangia mfuko huo ili ukue na uwe msaada mkubwa kwa wanahabari wote waliopo chini ya MPC.

Nae Mwenyekiti wa MPC Bwana Edwin Soko ameishukuru Desk & Chair Foundation kwa kuchangia mfuko huo wa solidarity Fund na kusema lengo la mfuko huo ni kusaidia waandishi wa habari kwenye huduma za kijamii.

Soko amewakumbusha pia wanachama wa MPC kuchangia mfuko huo ili baadae waanze kunufaika kwa kukopeshwa pale watakapohitaji.

No comments