Breaking News

Mgogoro wa kibiashara umetajwa kuwa chanzo cha mauaji

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ramadhani Ng'anzi akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano Leo hii januari 24,2022.

Na Hellen Mtereko, Mwanza

Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza limebainisha chanzo cha vifo vya watu watatu wa Familia moja  waliouwawa kwa kukatwa mapanga vichwani na shingoni Mkoani hapa Januari 18,2022 kuwa ni mgogoro wa kibiashara.

Kamanda wa  Polisi  Mkoani Mwanza Ramadhan Ng'anzi ameelezea chanzo cha vifo vya wanawake watatu  alipokuwa akizungumza na  vyombo vya habari leo hii ofisini kwake ambapo amesema  kuwa, mgogoro huo ni Kati ya marehemu hao na baadhi ya watuhumiwa wanaoshikiliwa na jeshi la Polisi.

Jeshi la Polisi lilipokea taarifa za tukio na lilianza upelelezi wa kina ambapo kuanzia januari 19, 2022  hadi  januari 23  jumla ya watuhumiwa wa tano walikamatwa  wakiwa na vielelezo mbalimbali zikiwemo mali za marehemu ambazo ziliporwa baada ya tukio hilo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ramadhani Ng'anzi akionyesha Mali za Marehemu ambazo ziliporwa baada ya tukio la mauaji ya watu watatu wa familia moja.

Aidha, Kamanda amesema kuwa  waliouwawa katika tukio hilo ni Marry Charles (42) ambae alikuwa mfanya biashara na mkaazi wa Mecco Wilaya ya Ilemela mama wa familia ,Jenifa Fredy (22) mkulima na Monica Jonas(19) ambae alikuwa ni msaidizi wa kazi za ndani wa familia hiyo.

Amesema jeshi la Polisi linaendelea kuwasaka watuhumiwa ambao bado hawajakamatwa, huku  akisema kuwa walifanya mahojiani na watuhumiwa ambao wamekwisha kamatwa na wamekili kutenda tukio Hilo kwa kutumia siraha aina ya panga.

"Vielelezo ambavyo watuhumiwa hao walivyo kamatwa navyo ni Friji aina ya Kyoto,Godoro moja lenye ukubwa wa 4 kwa 6 ,Tv mbili aina ya Singsung zote Nchi 18,radio mbili 2 aina  ya Seapiano na Alpu, Jiko moja la gesi aina ya Nikle pamoja na simu tatu aina ya Tecno zilizopatikana nyumbani kwa mmoja wa watuhumiwa maeneo ya Buhongwa",amesema Ng'anzi

Mwisho Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linawashukuru Wananchi  kwa ushirikiano wao katika kutoa taarifa za uhalifu, Jeshi linatoa wito kwa watu wenye kujihusisha na vitendo vya kihalifu kuwa Sheria itachukua nafasi yake.

Mwishoooooo

No comments