Breaking News

DIT yaendelee kutoa Hamasa kwa Watoto wa kike Kusoma Sayansi


Na Maridhia Ngemela, Mwanza

Taasisi ya Sayansi na Tekinolojia imewafikia wanafunzi wa kike wa sule za Sekondari elfu 5000 kwa lengo la kuwahamasicha kusoma masomo ya Sayansi.

Elimu hiyo imetolewa mikoa mbalimbali hapa Nchini ambapo leo Juni 16 Mwaka huu Taasisi hiyo imewakutanisha wanafunzi wa Sekondari Magu na Itumbili zilizopo Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza kwa lengo la kuhamasishwa kusoma masomo ya Sayansi ilikujiinua kiuchumi na kupata wabobezi wa masomo hayo.
 
Aneth Butashi na Grace Charles ni miongoni mwa wanafunzi waliohudhuria kikao cha kuwahimiza wanafunzi wa kike kusoma masomo ya Sayansi kilichofanyika leo June 16 Mwaka huu ambao wanatokea shule za Sekondari Magu na Itumbili zilizopo Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza wameiomba Taasisi ya DIT kuendelea kutoa elimu na kuwasisitiza wasichana kusoma masomo ya Sayansi ili kuwa na wahandisi,Madaktari na wabunifu wa kisayansi Nchini.

Wanafunzi hao wameiomba DIT kuendelea kusambaza elimu hiyo vijijini ili kuwazindua wazazi na wanafunzi ambao bado wanadhana ya kuwa masomo hayo yanasomwa na wanaume pekee na jamii kuondokana na mawazo hayo.

Hata hivyo Mkuu wa kitengo cha udahili kutoka Taasisi ya Sayansi na Tekinolojia (DIT) Dkt. Triphonia Ngailo alisema kampeni hiyo ya kuhamasisha wanafunzi wa kike kusoma masomo ya Sayansi ilizinduliwa mwaka Jana Octoba mpaka sasa wamefikia wanafunzi elfu 5,000 mpaka sasa ikiwa ni lengo la kuwahamasicha ili wamalizapo masomo yao wakajiunge katika chuo hicho kutokana na uwepo wa wanafunzi wa kike kuwa mdogo hivyo wanaendelea kuwatia hamasa katika sekta ya Sayansi na Tekinolojia.

Dkt.Ngailo alisema kuwa,katika kampeni hiyo wamepata mafanikio makubwa kutoka kwa wasichana ambao wanajaza fomu za kujiunga katika chuo hicho kutokana na kampeni hiyo na wanatembea na wanawake wahandisi ambao ni wabobezi katika hesabu,kemia ikiwa ni njia moja wapo ya kuwaonesha kuwa wanaweza kusoma na kufanikiwa kupitia wao na kusoma masomo hayo.

"Tumebaini changamoto kubwa ni watoto kutoona wanawake ambao wamefanikiwa kupitia masomo ya Sayansi na Shule nyingi ambazo tumepita hazina taarifa sahihi ya chuo cha DIT kuwa kinatoa masomo ya kisayansi inapelekea wao kumaliza masomo yao na kushindwa kutambua kuwa Kuna chuo hiki"alisema Ngailo.

Alisema kuwa,kampeni hiyo italeta matunda makubwa kwa watoto wa kike na lengo kubwa ni kuongeza udahili katika masomo hayo ameongeza kuwa changamoto walizobaini ni umbali uliopo kwa shule kutokana na mazingira ambayo yanawakwamisha watoto wa kike na kusababisha kukatisha masomo yao kutokana na vishawishi wanavyokutana navyo njiani pindi waedapo shuleni.

Afisa elimu taaluma kutoka Wilaya ya Magu aliyekuwa amemuwakilisha Mkurugenzi wa Magu Faraja Ndaro amesema Wilaya hiyo inamkakati wa kuwahamasicha watoto wa kike kusoma masomo ya Sayansi na kupitia elimu waliyoipata kupitia kampeni hiyo ambayo imetolewa na wataalamu kutoka DIT itaongeza hamasa zaidi na kuona umuhimu wa kusoma masomo hayo kutokana na wanaotoa elimu hiyo ni wanawake walosoma masomo ya Sayansi.

Hata hivyo Makamu Mkuu wa shule ya Magu Sekondari Mathew Kibuta amethibitisha kutokuwepo ufaulu mzuri kwa watoto wa kike katika masomo ya Sayansi kutokana na dhana ambayo inawapotosha kuwa masomo hayo ni magumu na kupata muitikio mdogo.

Alisema kuwa mfumo dume bado upo hata katika masomo na kupelekea watoto hao kutoyapa kipaumbele na kuona kuwa wao hawayawezi na kuwaachis wanafunzi wa kiume na ameiomba Serikali kuwaongezea walimu wakike katika masomo ya Sayansi ilikuendelea kuwahamasicha zaidi.

 Mpaka sasa wamefikia shule 12 za sekondari na Kampeni hiyo inatarajia kumalizika June 17 mwaka huu katika Mkoa wa shinyanga .

No comments