Breaking News

SHIRIKA LA DWWT LATOA TUZO KWA WANAWAKE NA WASICHANA WAVIU

Tonny Alphonce,Dar es Salaam 

Shirika la Dignit and wellbeing for women living with hiv in Tanzania (DWWT) limeombwa kuendelea kuwatambua na kuwapa moyo wa kufanyakazi kwa bidii wanawake na wasichana ambao wanapambana na changamoto za UKIMWI nchini. 

Kauli hiyo imetolewa na mratibu wa UKIMWI jijini Dar es Salaam Grace Kessy ambae alikuwa mgeni rasimi katika sherehe za kuwapongeza na kuwapa tuzo za F.I.E.R.C.E wanawake na wasichana WAVIU kutokana na mafanikio na kazi nyingi walizofanya katika mwitikio wa VVIU na UKIMWI nchini.

Grace amesema mafanikio makubwa yameonekana kwa upande wa VVU na UKIMWI kutokana na jitihada na kazi zinazofanywa na wanawake na wasichana katika jamii ya watanzania na kupelekea watu wanaoishi na VVU kuwa na matumaini ya kuendelea kuishi na wengine wakihamasika kupima afya zao. 

“Tunatambua umuhimu wa ushirikiano kati ya mashirika yasiyo ya kiserikali na leo napenda kuwashukuru DWWT kwa jitihada zao za kipekee katika kuboresha afya na ustawi wa wanawake wanaoishi na VVU”.alisema Grace 

Kwa upande wake mjumbe wa bodi ya DWWT Veronica Joseph amesema lengo la kuanzishwa shirika la DWWT ni kuwajengea uwezo wanawake na wasichana WAVIU katika kutetea na kukuza mahitaji na haki zao wenyewe pamoja na kuwa na jamii inayoheshimu na kutoa ushirikiano wa upatikanaji wa haki na huduma kwa wanawake na wasichana WAVIU katika ngazi zote. 

“Tukio la leo ni ushahidi wa nguvu za wanawake na wasichana katika mapambano ya VVU na UKIMWI katika Nyanja zote kuanzia kinga,tiba na matunzo maeneo hayo mmeyafanyiakazi vilivyo na mnastahili kupata tuzo hizi.”alisema Veronica 

Nae Rustika Banzi ambaye ameshinda tuzo na kupata nafasi ya kuiwakilisha DWWT nchini Uganda amewashukuru wale wote waliompigia kura na kuibuka mshindi huku akitoa ahadi ya kuendelea kuwa saidia WAVIU kuanzisha miradi ya kiuchumi pamoja na kuendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa kutumia dawa za ARV kwa usahihi.

Utoaji wa tuzo hizo za F.I.E.R.C.E. uliandaliwa na shirika la DWWT kwa udhamini wa Jumuiya ya kimataifa ya wanawake waishio na VVU ukanda wa Afrika Mshariki (ICWEA) ka kutolewa katika ofisi za NACOPHA makao makuu jijini Dar es Salaam tarehe 19/05/2023.

No comments