Breaking News

RC KILIMANJARO AIPONGEZA SIHA KWA KUSIMAMIA VYEMA FEDHA ZA UJENZI

Na Tonny Alphonce,Siha

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Nurdin Babu Leo 16 Agosti,2023 atoa pongezi kwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Siha na Uongozi wa Halmashauri kwa usimamizi bora wa ujenzi wa Mabweni na Madarasa ya Kidato cha Tano mwaka 2023.


Pongezi hizo amezitoa leo katika shule ya Sekondari Oshara alipokuwa akikagua ujenzi wa Mabweni Mawili Madarasa 7 na matundu 14 ya vyoo kwa fedha shilingi milioni 464.4 kutoka Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Napenda kuwapongeza sana Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha chini ya Uongozi wa Mwenyekiti wa Halmashauri pamoja na Mkurugenzi kwa kusimamia vizuri ujenzi unaondelea" alisema Mhe.Nurdin Babu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Siha amesema ujenzi huo wa Mabweni na Madarasa ya kidato cha tano utasaidia wanafunzi wanaotoka mbali kupata eneo zuri la kulala na hivyo kusoma bila tatizo lolote.


No comments