Breaking News

RITA YAPEWA KONGOLE USAJILI, ELIMU MAONESHO NANE NANE 2023


Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Bw. Frank Kanyusi akimkabidhi cheti cha kuzaliwa mmoja wa wananchi kwenye maonesho ya kimataifa ya kilimo Nane Nane katika viwanja vya John Mwakangale Mkoani Mbeya

 *****
Wananchi Mkoa wa Mbeya na Maeneo ya Jirani wameipongeza RITA kwa Kutoa Elimu,kufanya Usajili na Kutoa Vyeti vya kuzaliwa kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane 2023 katika viwanja vya John Mwakangale Mkoani Mbeya.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti wananchi hao wamesema kuwa wamenufaika pakubwa kwa Elimu kuhusiana Wosia na mambo ya Ndoa huku wakiisifu zaidi kwa kuwapatia vyeti vyao hapo hapo kwenye maonesho hayo.

"Mimi nilipata ruhusa ya siku mbili nikasema nikajaribu kufuatilia japo sikua na uhakika lakini nashukuru Mungu nmepata cheti changu hiki hapa sahizi naenda kuomba zangu Chuo",amesema Anita Mwakilasa mmoja wa wananchi waliopata cheti Nanenane.

"Siku zote Huwa nasema ntaandika kesho kesho lakini nawapongeza hawa RITA wamenielimisha kwanza Wosia sio Uchuro na Wosia ni siri sasa nina amani na nitaenda waniandikie", ameongeza Stani Ngimba.

Aidha Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Bw. Frank Kanyusi na Naibu Kabidhi Wasii Mkuu Bi. Irene Lesulie wameshiriki kilele cha Maonesho ya kimataifa ya Kilimo ya nane nane kitaifa mkoani Mbeya Pamoja na mambo mengine viongozi hao walishiriki katika kutoa huduma na kukabidhi vyeti vya kuzaliwa kwa wananchi katika Banda la Wakala.

No comments