Breaking News

HABARI PICHA:NELICO YAUTAMBULISHA MRADI WA URAIA WETU

Na Tonny Alphonce,Mwanza

Azaki ya New Light Children Centre Ogarnization NELICO leo tarehe 29/09/2023 imezindua mradi wa Uraia Wetu unatakaotekelezwa kwa miaka mitatu katika mikoa ya Mwanza,Geita,Kagera,Shinyanga,Simiyu na Mara.

Mradi huu wa Urai Wetu  unalenga kutengeneza mahusiano mazuri  baina ya serikali na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ili kuweza kutatua changamoto zinazotokana na uendeshaji wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali katika sheria ,kanuni na taratibu zinazoongoza mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ili kuondoa changamoto zilizopo hivyo kuweka nguvu ya pamoja kati ya serikali na wakuu wa mashirika ili waweze kuwa na ajenda ya pamoja.

Afisa Mradi wa Uraia Wetu kutoka NELICO akielezea lengo la mradi wa Uraia Wetu mradi ambao unaigusa mikoa ya Mwanza,Geita,Kagera,Shinyanga,Simiyu kwa kuzijengea uwezo AZAKI katika utendaji wao wa kazi za kila siku katika maeneo ya Utawala Bora na Democrasia kwa ujumla wake.

Kaimu mkurugenzi mtendaji wa NALICO akifungua kikao cha utambulishaji wa mradi wa Urai Wetu ambapo aliwakumbusha wakurugenzi wa mashirika kuwa baada ya miaka mitatu watapimwa kuona namna gani mradi umeweza kuleta mabadiliko katika utendaji kazi wa mashirika yaliyoshirikishwa katika mradi.

Yusuph Omolo Okoko afisa msajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali manispaa ya Ilemela akielezea mahusiano yaliyopo kati ya serikali na mashirika yasiyokuwa ya kiserika ambapo ameyataka mashirika hayo kufuata sheria na kanuni zilizopo katika kuendesha mashirika yao lakini pia ameyataka mashirika hayo kutumia majukwaa yao ya kisheria kutatua changamoto zilizopo.

Baadhi ya washiriki wa semina ya siku moja iliyofanyika leo jijini Mwanza wakifatilia maelezo kuhusu mradi wa Urai Wetu uliotambulishwa na NALICO.

Baadhi ya washiriki wa semina ya siku moja iliyofanyika leo jijini Mwanza wakifatilia maelezo kuhusu mradi wa Urai Wetu uliotambulishwa na NALICO.


Baadhi ya washiriki wa semina ya siku moja iliyofanyika leo jijini Mwanza wakifatilia maelezo kuhusu mradi wa Urai Wetu uliotambulishwa na NALICO.

No comments