WANACHAMA WA TMFD WANOLEWA NA EMEDO JUU YA MRADI WA KUZAMA MAJI KWA WAVUVI
Na Tonny
Alphonce,Dodoma
Waaandishi wa habari za Uvuvi na Wanachama wa Taasisi ya waandishi wa habari ya kuendeleza shughuli za Bahari na Uvuvi(TMFD) wamepatiwa mafunzo ya siku moja na shirika la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo juu mradi wa kuzuia kuzama majini katika ziwa Victoria.
Waandishi wa habari za kuendeleza shughuli za Bahari na Wavuvi wakiwa katika picha ya pamoja
Waandishi hao
waliopatiwa mafunzo hayo wametoka katika mikoa ya Mwanza,Dar es
Salaam,Geita,Kagera na Pwani ambapo pia wajulishwa juu ya mtandao wa kimataifa wa kuzuia kuzama maji Tanzania.
Akizungumza katika
warsha hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa TMFD Edwin Soko amewapongeza waandishi hao
wa habari kwa kuanza kubobea kwenye uandishi wa habari za aina moja ambao
utasaidia habari nyingi kuandikwa kwa kina.
Soko amesema ili waandishi waweze kuhamasika zaidi TMFD imeanza mchakato wa kuhakikisha habari Uvuvi zianze kushindanishwa na washindi waweze kupatiwa zawadi.
Akizungumzia
mradi wa kuzuia kuzama maji unaotekelezwa na EMEDO,Soko amesema kwa waandishi wa habari za uvuvi kushiriki katika kuufahamu mradi huo ili
waweze kuujulisha Umma hasa wavuvi juu
ya umuhimu wa kuchukua tahadhari wanapokuwa majini.
No comments