Breaking News

MASHINDANO YA MBIO ZA BAISKELI ZA CRDB YAONGEZA SHANGWE KUMBUKUMBU YA BABA WA TAIFA

 


Wanawake waendesha baiskeli wakizunguka uwanja wa CCM Kambarage mara 30 ambapo mshindi wa kwanza ni Kipepeo Futi Mbili
Mbio za baiskeli zikiendelea katika uwanja wa CCM Kambarage

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Tamasha la Mbio za Baiskeli Shinyanga lililoandaliwa na Benki ya CRDB ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Kumbukumbu ya Siku ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere limehitimishwa kwa kishindo mkoani Shinyanga ambapo washindi wa mbio hizo wameondoka na zawadi nono ya Shilingi Milioni 7.2 huku unit zaidi ya 500 za damu salama zikipatikana.


Tamasha hilo limefanyika leo Jumamosi Oktoba 14,2023 katika Uwanja wa CCM Kambarage  Mjini Shinyanga likihusisha uchangiaji damu salama pamoja na burudani pendwa ya mbio za baiskeli kwa makundi ya wanaume na wanawake.

Akizungumza kwenye kilele cha Mbio za Baiskeli za CRDB Shinyanga (Shinyanga CRDB Cycling Rally) , Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Prof. Siza Tumbo akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme, ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuandaa tamasha hilo kwa ajili ya kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akisema zimesaidia kuutangaza mkoa huo na kufungua zaidi fursa za kiuchumi na uwekezaji.


“Maadhimisho ya Sisi Shinyanga tunaadhimisha Kumbukumbu ya Siku ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika kumuenzi Baba wa Taifa ikiwa ni pamoja na hitimisho la mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023. Wananchi changamkieni fursa zinazotolewa katika Benki ya CRDB”,amesema.
Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Prof. Siza Tumbo akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme.

“Mbio hizi sio tu zinatoa fursa kwa wananchi wanaoshiriki kuimarisha na kulinda afya zao, bali washindi wanapata zawadi zinazowahamasisha wao na wengine kuendelea kushiriki mbio hizi. Baada ya mbio hizi ambazo zimepata umaarufu mwaka hadi mwaka zikifanyika kwa mafanikio kwa miaka minne sasa, tunaamini kabisa kwamba iwapo utafiti utafanyika leo hii, hatutashangaa kusikia Mkoa wa Shinyanga unaongoza kwa idadi kubwa ya baiskeli jambo ambalo litakuwa limechangiwa na Benki ya CRDB”,amesema Prof. Tumbo.

“Mbio hizi zimetoa fursa ya kuutangaza mkoa wetu pamoja na kufungua fursa za kiuchumi kwa wananchi na wafanyabiashara. Kadri miaka inavyozidi Kwenda, umaarufu wa mbio hizi unazidi kuongezeka hivyo basi, wakati Benki ya CRDB ikifungua njia, naziomba kampuni nyingine nazo kuangalia namna ya kufungua fursa za mkoa wetu huu jambo litakalosaidia kuboresha maisha ya wananchi,” ameongeza.

Endapo mbio hizo zitaendelezwa na kuwakaribisha washiriki kutoka kote nchini hata nje ya mipaka ya Tanzania, amesema anaamini zitaitangaza vyema Shinyanga na kutoa fursa kwa vijana kushiriki mashindano ya aina hiyo kimataifa jambo litakaloimarisha kipato chao.
Kabla ya kuhitimishwa kwa mbio hizo, zilitanguliwa na shughuli za kijamii ikiwamo kuchangia damu ambapo zaidi ya chupa 500 za damu salama zimekusanywa kwa ajili ya wagonjwa wenye uhitaji wanaotibiwa katika hospitali na vituo vya afya mkoani humo na nchini kote kwa ujumla.

Katika hotuba ya Meneja wa Benki ya CRDB kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana iliyosomwa na Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga ,amesema mbio hizo hufanyika kila mwaka siku ya kumbukumbu ya baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambaye alipenda kila mwananchi kuwa huru kiuchumi kwa kujituma kufanya kazi kulingana na fursa zilizopo kwenye eneo alilopo.

Amesema Benki ya CRDB ni mdau mkubwa wa michezo nchini kutokana na imani kubwa kwamba inajenga ushirikiano, mshikamano, na kuwaleta watu pamoja hivyo kuwa rahisi kuleta maendeleo katika jamii.

“Baada ya kuimarisha afya kitu muhimu ni kuwa na uchumi imara. Benki ya CRDB inayo zaidi ya matawi 260 nchini kote ambako wananchi wanaweza kuyatumia kuzichangamkia fursa walizonazo. Mtu mwenye afya njema tayari anao mtaji wa kuanzia kufanikisha mlengo yake. Naomba tuendelee kujitokeza kwenye michezo mbalimbali inayofanyika kwenye maeneo yetu kwani iasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha afya,” ameongeza.

Licha ya mbio hizo za baiskeli, Benki ya CRDB pia huandaa na kusimamia mbio za kimataifa zijulikanazo kama CRDB Bank Marathon huku ikidhamini mingine kadhaa zikiwamo jezi za Zanzibar Heroes, Simba Day na Wiki ya Mwananchi, na ni mfadhili timu ya Namungo inayoshiriki Ligi Kuu Bara na inadhamini Mashindano ya CRDB Bank Ngalawa Race yanayofanyika Kizimkazi visiwani Zanzibar. 

Amefafanua kuwa , Katika kuwezesha shughuli za kiuchumi, kuanzia Aprili mwaka jana mpaka sasa hivi, Benki ya CRDB imekopesha zaidi ya shilingi bilioni 6 kwa wachimbaji wadogo wa madini mkoani Shinyanga huku shilingi bilioni 65.3 zikielekezwa kwenye kilimo hasa cha mpunga na pamba hivyo kuwesha ununuzi wa zana za kilimo, pembejeo pamoja na kuimarisha masoko ya mazao yanayovunwa kila mwaka. Vilevile, kupitia mradi wa Keti Jifunze inaoutekeleza nchini kote, imetoa madawati 250 katika shule mbili za msingi na sekondari moja ili kuboresha mazingira ya kujifunzia. 

“Benki yetu pia inayo programu ya Imbeju inayotoa mtaji wezeshi kwa vijana na wanawake. Fursa hii ni kwa ajili ya watu wote tukiwamo wakazi wa Shinyanga na vitongoji vyake. Nawakaribisha vijana wenye mawazo na miradi yenye ubunifudani yake pamoja na wanawake mliopo kwenye vikundi vinavyojihusisha na masuala ya ujasiriamali, tunazo fursa kwa ajili yenu,” amesisitiza . 


Katika Mashindano hayo, jumla ya shilingi Milioni 7.2 zimetolewa na Benki ya CRDB kama zawadi washindi wa mbio za baiskeli wa kwanza hadi wa 10 katika makundi ya wanaume na wanawake ambapo kwa upande wa Wapanda Baiskeli Wabobezi waliokimbia Km 150 kutoka Kambage Shinyanga Mjini hadi Isaka Kahama na kurudi mshindi wa kwanza ni Kulwa Gelard aliyeondoka na kitita cha shilingi Milioni 1.5.
Mshindi wa Kwanza , Makirikiri Joseph akimaliza kwa kupiga saluti mbio za kundi la Wanawake waendesha baiskeli wakiwa na ndoo kichwani waliozunguka uwanja wa CCM Kambarage mara 10

Nao wapanda Baiskeli wanaochipukia waliokimbia Km 100 mshindi wa kwanza ameibuka na kitita cha shilingi 700,000 na wapanda baiskeli wakongwe mshindi wa kwanza ameondoka na zawadi ya shilingi 150,000/=, wanawake wanaokimbia na ndoo za maji kichwani waliozunguka uwanja wa CCM Kambarage mara 10 mshindi wa kwanza Makirikiri Joseph akiondoka na zawadi ya shilingi 30,000/= na wanawake waliozunguka uwanja wa CCM Kambarage mara 30 mshindi wa kwanza Kipepeo Futi mbili aliyeondoka na kitita cha shilingi 500,000/=.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Prof. Siza Tumbo akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme kwenye kilele cha Mbio za Baiskeli za CRDB Shinyanga (Shinyanga CRDB Cycling Rally) leo Jumamosi Oktoba 14,2023 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney akizungumza kwa niaba ya Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana kwenye kilele cha Mbio za Baiskeli za CRDB Shinyanga (Shinyanga CRDB Cycling Rally) leo Jumamosi Oktoba 14,2023
Meneja  Mahusiano Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi , Deogratius Mambo akizungumza kwenye kilele cha Mbio za Baiskeli za CRDB Shinyanga (Shinyanga CRDB Cycling Rally) 
Mwneyekiti wa Cha Baiskeli Mkoa wa Mwanza, Elizabeth     Sospeter Sayayi akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Chama Cha Baiskeli Taifa kwenye kilele cha Mbio za Baiskeli za CRDB Shinyanga (Shinyanga CRDB Cycling Rally)
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Prof. Siza Tumbo ( wa kwanza kushoto) akifuatilia Mbio za Baiskeli za CRDB Shinyanga (Shinyanga CRDB Cycling Rally)
Wadau wakifuatilia Mbio za Baiskeli za CRDB Shinyanga (Shinyanga CRDB Cycling Rally)
Waendesha baiskeli Chipukizi wakimaliza Mbio za Baiskeli Km 100
Mshindi wa kwanza mbio za Baiskeli kundi la Wabobezi Kulwa Gelard akimaliza mbio za Km 150
Wanawake waendesha baiskeli wakizunguka uwanja wa CCM Kambarage mara 30 ambapo mshindi wa kwanza ni Kipepeo Futi Mbili
Mbio za baiskeli zikiendelea katika uwanja wa CCM Kambarage
Mbio za baiskeli zikiendelea katika uwanja wa CCM Kambarage
Wanawake waendesha baiskeli wakiwa na ndoo za maji kichwani wakizunguka uwanja wa CCM Kambarage mara 10.
Mshindi wa Kwanza , Makirikiri Joseph akimaliza kwa kupiga saluti mbio za kundi la Wanawake waendesha baiskeli wakiwa na ndoo kichwani waliozunguka uwanja wa CCM Kambarage mara 10
Mbio za baiskeli zikiendelea
Wadau wakifuatilia Mbio za baiskeli 
Wadau wakifuatilia Mbio za baiskeli 
Wadau wakifuatilia Mbio za baiskeli 

Wadau wakifuatilia Mbio za baiskeli 
Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Prof. Siza Tumbo akimpatia cheti cha shukrani Mwenyekiti wa Chama cha Baiskeli Mkoa wa Shinyanga Salula Gacha kuwa mdau mkubwa katika mchezo wa baiskeli  wakati wa kilele cha Mbio za Baiskeli za CRDB Shinyanga (Shinyanga CRDB Cycling Rally) leo Jumamosi Oktoba 14,2023
Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Prof. Siza Tumbo akikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza wa mbio za baiskeli Kulwa Gelard kundi la wanaume waliokimbia mbio za Km 150. Kulwa Gelard ameondoka na kitita cha shilingi Milioni 1.5
Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Prof. Siza Tumbo akimvalisha medali ya dhahabu na kukabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza wa mbio za baiskeli Kulwa Gelard kundi la wanaume waliokimbia mbio za Km 150. Kulwa Gelard ameondoka na kitita cha shilingi Milioni 1.5
Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Prof. Siza Tumbo akikabidhi zawadi kwa washindi wa mbio za baiskeli kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme
Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Prof. Siza Tumbo akikabidhi zawadi kwa washindi wa mbio za baiskeli kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme
Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Prof. Siza Tumbo akikabidhi zawadi kwa washindi wa mbio za baiskeli kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme
Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Prof. Siza Tumbo akikabidhi zawadi kwa washindi wa mbio za baiskeli kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme
Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Prof. Siza Tumbo akikabidhi zawadi kwa washindi wa mbio za baiskeli kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme
Zoezi la uchangiaji damu slama likiendelea katika uwanja wa CCM Kambarage
Mratibu wa Damu Salama Mkoa wa Shinyanga Dkt. Joel Mbale (kushoto) akimwelezea  Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Prof. Siza Tumbo kuhusu zoezi la uchangiaji damu salama lilivyofanyika kupitia Benki ya CRDB
Zoezi la utoaji huduma za kufungua Akaunti za CRDB likiendelea katika uwanja wa CCM Kambarage
Zoezi la utoaji huduma za kufungua Akaunti za CRDB likiendelea katika uwanja wa CCM Kambarage
Zoezi la utoaji huduma za kufungua Akaunti za CRDB likiendelea katika uwanja wa CCM Kambarage
Maafisa kutoka Chama cha Msalaba Mwekundu (Red Cross) wakiwa katika uwanja wa CCM Kambarage
Picha za kumbukumbu zikipigwa kwenye kilele cha Mbio za Baiskeli za CRDB Shinyanga (Shinyanga CRDB Cycling Rally)
Picha za kumbukumbu zikipigwa kwenye kilele cha Mbio za Baiskeli za CRDB Shinyanga (Shinyanga CRDB Cycling Rally) leo Jumamosi Oktoba 14,2023 - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

No comments