Breaking News

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YARIDHISHWA NA MAELENDELEO YA MRADI WA EASTRIP (DIT)-MWANZA

 

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imeeleza kuridhishwa na maendeleo ya mradi wa kujenga ujuzi kwa maendeleo na uingiliano wa kikanda katika Afrika Mashariki (EASTRIP) , unaotekelezwa katika Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam  (DIT), Kampasi ya Mwanza.



Awamu ya kwanza ya mradi huo unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa zaidi ya Sh billion 37, inahusisha majengo ya utawala,taaluma na mabweni mawili, miundombinu ambayo ujenzi wake umefikia zaidi ya asilimia 95.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Husna Juma, amesema kukamilika kwa mradi huo  kunafaida lukuki, ikiwemo kuchochea matumizi mazuri ya ngozi, ikizingatiwa Kanda ya Ziwa ni moja ya maeneo yenye mifugo mingi nchini.

"Kwa kawaida tumekuwa tukila nyama tu ngozi tunatupa, huku tukinunua bidhaa za ngozi kutoka nje. Sasa Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan ametuletea mradi huu wenye faida nyingi, ikiwemo kutengeneza ajira miongoni mwa wahitimu, iwe kuajiriwa au kujiajiri",.amesema Husna.

"Ujenzi wa majengo unakwenda vizuri na tuna imani utakamilika mwezi ujao kama makubaliano ya mkataba yanavyosema," amemaliza kwa kusema hivyo Mwenyekiti Husna.

 

No comments