Breaking News

HALMASHAURI NCHINI ZATAKIWA KUTENGA BAJETI YA PJT-MMMAM

 Na Tonny Alphonce, Dodoma

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt Doroth Gwajima amewataka wakurugenzi wote wa halmashauri nchini kuhakikisha wanapata bajeti ya kutekeleza Mpango wa Taifa wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt Doroth Gwajima akifungua rasimi mkutano wa kitaifa wa wadau watekelezaji wa Program Jumuishi ya kitaifa ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto

Dkt Gwajima ameyasema hayo leo tarehe 11/12/2023 mjini Dodoma alipokuwa akifungua mkutano wa kitaifa wa wadau watekelezaji wa Program Jumuishi ya kitaifa ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto.

Amesema programu hiyo ni muhimu kwa ukuaji timilifu wa mtoto na mkurugenzi atakayeshindwa kupata bajeti hiyo atakuwa anachangia sababu zinazoweza kusababisha mtoto asiweze kukua katika utimilifu wake.


“Ndugu zangu nimejaribu kujizungusha zungusha hapa lakini nimeshindwa naomba niagize tu moja kwa moja kwamba kila halmashauri ihakikishe inapata bajeti ya kutekeleza programu hii, bahati nzuri TAMISEMI wapo hapa pia wamesikia”.alisema Dkt Gwajima

Akizungumzia mkutano mkubwa wa maelezi makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto unaotarajiwa kufanyika mwezi wa tatu mwakani Dkt Ngwajima amewataka wadau wote wa afua za watoto wajiandae vema ili washiriki kutoka nchi za afrika mashariki waweze kujifunza kutoka Tanzania.

Awali akimkaribisha mgeni rasimi mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya waatoto kutoka wizara ya Maendeleo ya  Jamii, Jinsia Wazee, Wanawake na Makundi Maalumu Sebastian Kitiku amesema katika kuhakikisha maeneo matano ya ECD yanafanyiwa kazi ambayo ni Lishe, Afya Bora, Malezi yenye Mwitikio, Elimu na Ulinzi na Usalama wa Mtoto kwa uwiano wizara inampango wa kuanza kupima maeneo hayo kwa Score Card.

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya waatoto kutoka wizara ya Maendeleo ya  Jamii, Jinsia Wazee, Wanawake na Makundi Maalumu Sebastian Kitiku 

“Mheshimiwa Waziri hii Score Card itatusaidia kuhakikisha maeneo yote haya matano yanatekelezwa kwa uwiano sawa na kwa kufanya hivyo ni wazi kuwa mtoto atakua katika utimilifu wake”.alisema Mh Kitiku

Naye mkurugenzi mkazi kutoka Childrens in Crossfire Craig Ferla amesema hadi hivi sasa kuna maendeleo makubwa yameishapigwa katika halmashauri 114 tayari halmashauri 70 zimefikiwana programu hii.

Mkurugenzi mkazi kutoka Childrens in Crossfire Craig Ferla akielezea utekelezaji wa programu ya PJT-MMMAM

Craig ameiomba pia serikali kuangalia namna ya kupata bajeti itakayosaidia utekelezaji wa programu hii kwa kasi.

kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa The Union Of Tanzania Press Clubs (UTPC) Kenneth Simbaya amewataka wadau wa watoto kwa pamoja kuwatumia waandishi wa habari katika shughuli zao ili kuipa jamii haki ya kupata habari.

Mtendaji wa The Union Of Tanzania Press Clubs (UTPC) Kenneth Simbaya akielezea nafasi ya waandishi wa habari katika utekeleza wa programu ya PJT-MMMAM

"Waandishi wa habari wataendelea  kuchochea uwajibikaji na waandishi ndio daraja  la kuripoti ukweli na pale wanapowasema vibaya msichukie bali mfanyie kazi kile walichokiona kuwa hakijakaa vizuri".alisema Simbaya

Baadhi ya Washiriki wa kutano huo wa kitaifa wa wadau watekelezaji wa Program Jumuishi ya kitaifa ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto 

Mkutano huu wa kitaifa wa wadau watekelezaji wa Program Jumuishi ya kitaifa ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto ambao umewakutanisha Maafisa Ustawi wa Jamii, Maafisa Maendeleo ya Jamii, Viongozi wa CSOs na Waandishi Vinara wa habari za watoto umeanza leo tarehe 11/12/2023 na Utamalizika tarehe 14/12/2023 mjini Dodoma  ukiwa na lengo la kufanya tathimini ya Programu hii pamoja na kuzindua mpango maalumu wa utekelezaji wa programu hii.

 

No comments