Breaking News

MJUMBE WA MKUTANO MKUU CCM TAIFA AMIR MKUFYA (AMESCO) ATOA MSAADA WA VIFAA VYA SHULE KWA WANAFUNZI WALIOFAULU LUSHOTO

Na Tonny Alphonce, Tanga

Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa kutokea wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga  Amiri Mkufya (Amesco) ametoa msaada wa vifaa vya shule vyenye Thamani ya zaidi ya sh millioni tatu kwa watoto tisa waliofaulu kuingia kidato Cha kwanza mwaka 2024.

Vifaa hivyo vilivyotolewa na mjumbe  huyo wa Mkutano Mkuu CCM Taifa ni pamoja na Madaftali, kalamu, Masanduku ya kuhifadhia vifaa vya shule maarufu (Tranka) pamoja na nauli za kutoka lushoto na  kuwafikisha katika shule walizofaulu.

Mkufya amesema kuwa lengo la kutoa msaada huo ni kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya  Rais Samia za kuhakikisha Kila mtoto wa kitanzania anapata elimu.


"Vijana hawa wamefanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho na wamefaulu na mimi nimeguswa kuwasaidia ili waweze kutimiza ndoto zao licha ya familia zao kuonekana kushindwa kuwapeleka shule".alisema Mkufya

Akishukuru kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Mwanafunzi Benard Vicent James aliyemaliza shule ya msingi Kikumbi ambae amechaguliwa kwenda Tabora Boys kwa masomo ya kidato cha kwanza amesema msaada walioupata kutoka kwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa kutokea wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga  Amiri Mkufya   ni mkubwa na unaenda kutimiza ndoto zao.
Baadhi ya wazazi na walezi wakiangalia sehemu ya misaada iliyotolewa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa kutokea wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga  Amiri Mkufya

"Kiukweli nakosa neno zuri la kusema kuhusu msaada huu kwa sababu mimi hapa nilipo nimefiwa na baba na mamangu hana uwezo kwa maana hiyo licha ya kufaulu nisingeweza kuendelea na masomo kwasababu nyumbani hatuna pesa".alisema Benard
Baadhi ya wazazi na walezi wakiangalia sehemu ya misaada iliyotolewa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa kutokea wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga  Amiri Mkufya

Wanafunzi walionufaika na msaada huo ni wale wanaotoka katika familia duni na waliopata ufaulu wa alama A ,ambao wamechaguliwa katika shule za vipaji mbazo ni Tabora boys,Tabora gils,Tanga School, Shambalai sekondari,Balangdalau Sekondari, Makangali sekondari (Mufindi),Mwadui Tech iliopo shinynga na Moshi Tech .

No comments