Breaking News

JESHI LA MAGEREZA NCHINI LAJIPANGA KWA KILIMO, MAZAO YA ZIADA KUSAIDIA KADA ZINGINE

 Na Tonny Alphonce, Mwanza

Jeshi la Magereza nchini limesema katika msimu ujao wa kilimo limejipanga kuzalisha mazao ya muhimu kwa asilimia isiopungua 100 ya mahitaji ya jeshi la magereza na ziada itakayopatikana itapelekwa kwenye vyuo na sekondari za serikali.

Akizungumza katika zoezi la utoaji nishani kwa askari magereza 302 wa kanda ya ziwa tarehe 23/05/2024, kamishina Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP), Mzee Ramadhani Nyamka kwa niaba ya amiri jeshi mkuu rais Salimia Suluhu Hassan amesema mazao hayo muhimu wanayotarajia kuzalisha katika msimu ujao ni mahindi na mpunga wa kutosha ili kulisha magereza zote nchini na kupatikana ziada itakayosaidia kada zingine.

Amesema katika kuhakikisha uzalishaji unaongezeka jeshi la magereza tayari limeanzisha skimu za umwagiliaji katika baadhi ya magareza nchini ukiwemo mradi mkubwa wa kilimo cha mpunga katika gereza la idete mkoani morogoro ambapo ujenzi umefikia asilimia 70 na utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kutosheleza mahitaji ya jeshi la magereza kwa asilimia 80.

Kwa upande wa dhana ya urekebishaji wa wafungwa nchini amesema tayari jeshi la magereza nchini limechukua hatua ya kuimarisha programu za urekebu kwa kupitia upya mitaala na kupendekeza mitaala mipya ambayo imeishapelekwa kwenye mamlaka zinazo husika na zikipitishwa zitaanza kufanya kazi zikiwa na lengo la kuboresha program za urekebu zitakazowasaidia wafungwa wakitoka waweze kumudu maisha na kufanya shunguli za kiuchumi na kuchangia katika maendeleo ya taifa.

Nishani ambazo mheshimiwa rais amezitoa ni pamoja na nishani ya muungano daraja la nne,nishani ya utumishi uliotukuka,nishani ya utumishi wa muda mrefu na nishani ya nne ni nishani ya  utumishi wa muda mrefu na tabia njema.

Kanda ya ziwa ni kanda ya tatu katika mgawanyo ambao kamishina Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP), Mzee Ramadhani Nyamka amepanga kuwavisha nishani askari magereza kwa niaba ya mheshimiwa rais na amiri jeshi mkuu.

 

No comments