Breaking News

MWANDISHI MWANDAMIZI SOKO AWATAKA WAANDISHI WA HABARI KUANDIKA HABARI ZA VIFO VYA KUZAMA MAJI

 

Na Mwandishi wetu Dar

Hayo yamesemwa leo na mwandishi mwandamizi Edwin Soko alipokuwa  akiwafundisha wahariri wa vyombo vya habari wa Mkoa wa Dar es salaam kwenye mafunzo maalumu ya kuzuia  vifo vya kuzama maji yaliyoandiwa na Mamlaka ya hewa Nchini(TMA) kwa kushirikiana na EMEDO.


Soko aliwasisitiza waandishi wa habari hao kujenga ubobezi wa kuandika habari za kuzuia vifo vya maji ili jamii ipate kuelewa kwa upana vyanzo na namna ya kujikinga kwenye vifo vya kuzama maji.

Katika wasilisho lake Bwana Soko aliwafundisha waandishi hao njia na mbinu mbalimbali za kuandika habari zinazoweza kuleta mabadiliko ya kisera na kisheria na kupunguza idadi ya vifo .

Kwa upande wake Afisa program wa EMEDO bwana Arthur  Mugema  alisema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa kundi la waandishi wa habari kwa kuwa wana mchango mkibwa wa kufikisha habari kwa jamii kwa mara moja na hivyo kusaidia kupunguza vifo vinavyotokana na kuzama.maji.

Naye BIbi Angel Baruti Mwenyekiti wa mtandao wa kuzuia kuzama maji Tanzania, alisema kuwa mafunzo hayo yataongeza uelewa kwa waandishi wa habari wa namna ya kuandika vyema habari za vifo vya maji na kupunguza vifo hivyo.

Pia alisema kuwa wanataraji kuwa na tuzo  maalumu kwa waandishi wa habari watakaofanya vyema

Jumla ya waandishi wa habari 30 toka Jijini Dar es salaam walishiriki mafunzo hayo ya siku moja yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mbezi Garden Jijini Dar es salaam

No comments