Breaking News

Adam Natepe aachia ngazi ZFF

Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) limeridhia ombi la msemaji wake, Adam Natepe kujiuzulu katika nafasi yake kuanzia Jumatatu, Julai 6, 2020.

ZFF imesema kuwa mseamaji huyo ameamua kujiuzulu kutokana na sababu za kiafya pamoja na kubanwa na majukumu yake binafsi.

"ZFF itaendelea kuthamini mchango mkubwa alioutoa katika kupigania soka la Zanzibar kipindi chote ambacho alitumikia nafasi hiyo, hivyo ZFF itaendelea kuungana naye kimajukumu pale afya yake itakapoimarika", imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Adam Natepe amejizolea sifa katika soka la Tanzania siku za hivi karibuni hasa katika vyombo vya habari kutokana na msimamo wake wa kupigania haki za ZFF, mfano mzuri ni pale alipohitaji ufafanuzi wa mgao wa fedha kutoka Shirikisho la Soka Tanzania TFF.

Hii hapa ni taarifa rasmi ya ZFF.

No comments