Breaking News

UTPC yaahidi Milioni 100 kwa MPC


Mkurugenzi wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Abubakar Karsan ameahidi kusaidia upatikanaji wa Tsh. Milioni 100 kutoka kwa wadau mbalimbali ili kusaidi utekelezaji wa miradi wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza (MPC) ikiwemo ujenzi wa ofisi ya ghorofa tatu, uanzishaji wa redio pamoja na luninga ya mtandaoni.


Karsan aliyasema hayo Novemba 09, 2019 jijini Mwanza kwenye mkutano wa wasaa wa marafiki wa Habari Mkoa Mwanza ulioandaliwa na MPC akisisitiza kwamba kusudio hilo amekuwa nalo kwa muda mrefu hivyo ni furaha yake kuona linatimia.


Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko alisema mikakati ya kutekeleza miradi hiyo tayari imeanza ambapo tayari Luna kiwanja katika eneo la Isangijo wilayani Magu huku akipongeza ari ya wanachama wa chama hicho ambao tayari wameanza kutoa michango ya kila mwezi ili kupata fedha za kuanzia.


Mkutano huo ulifunguliwa na Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella ambaye ameahidi ushirikiano wa hali na Mali kwa MPC ili kufanikisha juhudi za kuchochea maendeleo mkoani Mwanza.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG


Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsani (katikati) akizungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella na kutoka kushoto ni Florah Magabe ambaye ni Katibu wa Mbunge wa Nyamagana pamoja na Mwakilishi kutoka NSSF, Felix Mbise.


Wanahabari na marafiki wa Habari mkoani Mwanza wakifiatilia mkutano huo.

Chanzo Cha Habari: BMG BLOG

No comments