Breaking News

VIONGOZI,WANANCHI WAFURIKA UWANJA WA MAGUFULI ULIOPO CHATONa Tonny Alphonce,Mwanza


Viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Hemed Suleiman Abdulla pamoja na wananchi tayari wamefika katika Uwanja wa Magufuli uliopo Chato mkoani Geita tayari kwa ajili ya kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.


Viongozi mbalimbali pamoja na wananchi kutoka mikoa ya kanda ya ziwa wameendelea kusogea katika Uwanja wa Magufuli kwaajili ya kuuaga mwili wa Hayati Magufuli.Zoezi la kuuga mwili wa Hayati Magufuli Chato litafanyika leo ambapo viongozi na wananchi watapata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho .
Hayati Dkt. Magufuli alifariki dunia Jumatano Machi 17, 2021 katika hospitali ya Mzena, Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu na anatarajiwa kuzikwa Ijumaa Machi 26 wilayani Chato mkoani Geita.No comments