Breaking News

Wavuvi katika eneo la Kigongo Ferry wasindikiza mwili wa Magufuli kwa mitumbwiEllukagha Kyusa ,BusisiMamia ya wananchi katika eneo la kivuko cha Busisi wametokwa na machozi wakati mwili wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano John Pombe Magufuli ukivushwa huku wavuvi wakiusindikiza kwa mitumbwi yao.Wavuvi hao ambao wengi walibeba picha za Magufuli na mabango yaliyoonyesha ushujaa wa Magufuli katika uongozi wake walioonekana kusikitika na kuamini kuwa Magufuli amefariki ikiwa watanzania wanamuhitaji.Baadhi ya waombelezaji ambao pia ni wakazi wa eneo la Kigongo ferry waliungana na wavuvi hao kwenye mitumbwi kuelekea upande wa pili wa Busisi, Wilaya ya Sengerema.Tukio hilo limeuzunisha watu wengi na kuleta picha halisi ya kila sekta imemlilia Magufuli kwa aina yake.Kuanzia asubuhi asubuhi ya leo wakati mwili unapokelewa Mwanza mamia ya wakazi wa Mwanza wamemuuaga Magufuli kwa kuonyesha ishara mbalimbali.Mazishi ya hayati Magufuli yanataraji kufanyika Machi 26 Nyumbani kwako Chato.

No comments