Breaking News

KUNDI LA PILI LA WATALII 137 KUTOKA ISRAEL LAWASILI NCHINI

 







KUNDI la pili la watalii 137 kutoka nchini Israel  limewasili nchini na watakuwepo nchini kwa siku 7, huku  kundi la awali la watalii 150 kutoka Israel wakimaliza salama utalii wao nchini

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TANAPA imeelezwa kuwa watalii hao wamefurahi mapokezi yaliyoandaliwa kwa ajili hayo na kuelezwa kuwa makundi mengi zaidi yanategemewa  kuwasili wiki ijayo na wengi wa watalii hao wakieleza namna  Tanzania ilivyobarikiwa vya kutosha huku wengi wao  wakiahidi kurudi tena na kusifu hatua zilizopo juu ya  tahadhari dhidi ya UVIKO 19.

No comments