Breaking News

Rc Gabriel:andaeni maeneo kwa wamachinga ambao hawajapata

Na Hellen Mtereko,MwanzaMkuu wa Mkoa wa Mwanza mhandisi Robert Gabriel ametoa wito kwa timu ya jiji wanaoratibu shughuli za upangaji wa  wamachinga kuhakikisha wanamaliza kazi hiyo haraka ili wamachinga waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku.

Hayo  aliyasema  ofisini kwake  wakati  akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mkoani hapa.

Alisema  amepokea maombi ya machinga  wanaofanya biashara zao kwenye maeneo ya  barabara ya soko la Buhongwa kuondoka maeneo yasiyo rasmi ifikapo Novemba 10 kwani watakuwa wameshakamilisha ujenzi wa vizimba katika maeneo waliyopangiwa.

Hata hivyo alisema  serikali imetoa maeneo bure ili  wafanyabiashara hao waweze  kujitafutia kipato.

"Mkibaini kuna watu,kikundi kinawaomba fedha ili mpate maeneo toeni taarifakwa uongozi ili tuweze kuwachukulia hatua za kisheria",alisema Gabriel

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Robert Gabriel akizungumza na wanahabari

Aidha, alilitaka shirika la umeme Nchini(TANESCO) kuhakikisha wanafanya taratibu za  kuweka umeme na kuainisha  maeneo ambayo wafanyabiashara hao watachukua umeme na kuingiza katika vizimba vyao.

Mwisho aliwaasa wamachinga kuendelea  kujikinga na ugonjwa wa uviko 19 sanjari na kupokea chanjo  mpya ambayo serikali ya Mkoa imepokea baada ya zile za awali kumalizia.


Mwishooooo

No comments