Breaking News

Wananchi wametakiwa kupata mafunzo ya usalama majini ili kupunguza ajali

Na Hellen Mtereko, Mwanza


Mkuu wa Jeshi la polisi Tanzania IGP Saimon Sirro akizungumza na maofisa wa Polisi Jijini Mwanza

Wananchi wanaoishi kando kando ya mto, ziwa na bahari wametakiwa kupata mafunzo ya usalama majini katika chuo cha Polisi wanamaji kilichopo Mkoani Mwanza ili kuweza kupunguza ajali za majini.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa jeshi la polisi Tanzania IGP Saimon Sirro wakati akizungumza na maofisa wa Polisi Jijini Mwanza katika kikao kazi kilicholenga kuimarisha utendaji kazi.

IGP Sirro alisema kuwa Wavuvi na wadau wengine wanaotumia vyombo vya majini watajengewa uwezo wa kukabiliana na ajali za majini ili kuweza kufanya shughuli zao kwa amani na salama.

" Niwasihi sana wale wote mnaotaka kujifunza mambo ya baharini waje kwenye chuo chetu cha wanamaji kilichopo hapa Mwanza kwani kimekubalika katika Nchi kumi na nne, na kwaupande wa gharama mafunzo yatatolewa kwa Bei nafuu sana",alisema Sirro


Mkuu wa Chuo cha Polisi wanamaji Mwanza,Kamishina msaidizi wa Polisi Ndagile Makubi

Kwaupande wake Mkuu wa Chuo cha Polisi wanamaji Mwanza Kamishina msaidizi wa Polisi Ndagile Makubi alisema kuwa mafunzo wanayoyatoa yatasaidia kuleta manufaa kwa Wavuvi na wanaojihusisha na kazi za Ziwani.

Alisema kuwa Chuo hicho kinatoa mafunzo ya wanamaji kwa askar wa Jeshi la Polisi,watumishi wa taasisi za umma na binafsi na kwa mtu mmoja mmoja, aliongeza kuwa mafunzo yanayotolewa ni ya usalama majini ambayo yatasaidia kuokoa watu pindi majanga yanapotokea.

"Majanga makubwa yamekuwa yakitokea Ziwani na baharini na watu wengi wanapoteza maisha, hii ni kwasababu watu wengi hawana ujuzi wakujiokoa  pindi majanga yanapowafika, ndio maana Chuo kimetoa fursa kwa mtu yoyote kuja kupata mafunzo ya kuogelea na ya uzamiaji",alisema Makubi

Mwishooooo

No comments