Breaking News

Dc Masala: wazazi kamilisheni mahitaji ya watoto ili waweze kujiunga na kidato Cha kwanza

Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya matokeo ya darasa la saba na ufaulu wa Wilaya hiyo.



Na Hellen Mtereko, Mwanza

Wazazi wametakiwa kufanya maandalizi mazuri ya watoto wao ya kwenda kujiunga na kidato chakwanza ili waweze kutimiza ndoto zao.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala wakatika akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya matokeo ya darasa la saba na mikakati waliyonayo  ya kuboresha ufaulu zaidi.

Masala amesema kuwa wazazi wanawajibu mkubwa sana wakujiandaa kikamilifu kwakuhakikisha mahitaji yote ya msingi kwa Watoto wao yanapatikana ikiwemo sare ya shule,viatu,madaftari,kalamu na begi ili Mtoto anapofika shuleni awe amekamilika.

Ameongeza kuwa kwahiki kipindi ambacho Watoto wanasubili kwenda kuanza masomo Ni vema wazazi au walezi waendelee kuwatunza na kuwafundisha watoto ili wasijiingize kwenye makundi ambayo si rafiki.

" Jitahidini sana kuwashauri na kuwatunza watoto kwakuangalia mienendo yao ya siku hadi siku na muwape nafasi ya kuwapeleka kusoma masomo andalizi ambayo yatawasaidia watakapokuwa wameanza kidato cha kwanza",

Akizungumzia ufaulu wa matokeo ya darasa la saba Masala amesema kuwa Wilaya ya Ilemela imekuwa ya saba kitaifa na ki Mkoa imekuwa ya pili,  ameongeza kuwa matokeo haya mazuri yametufanya  tuendelee kujipanga vizuri na kuweka mikakati ambayo itapelekea mwakani kuweza kushika nafasi ya kwanza Kitaifa.

Moja ya mkakati ambao tumeweka ni kuona ni kwanamna gani tunaboresha mazingira ya upatikanaji wa elimu bora katika Wilaya ya Ilemela kwa kuwa na madarasa ya kutosha na madawati ili Watoto waweze kukaa kwenye mazingira mazuri.

"Tumekuwa na utaratibu wa kuhakikisha tunajenga madarasa kuanzia Shule za msingi kwani tayari tunazo takwimu za madarasa yote ambayo yalikuwa bado hayajapauliwa ambayo tutakwenda kuyakamilisha.

Mwishooo

No comments