Breaking News

Takukuru yatoa tahadhari kwa wananchi kuepukana na matapeli


Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mwanza Frank Mkilanya akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake..

Na Hellen Mtereko, Mwanza

Wananchi Mkoani Mwanza wametahadharishwa kuepukana na matapeli wanaojifanya kuwa ni maafisa wa Takukuru badala yake wafike katika ofisi husika ili kuepuka usumbufu utakaoweza kujitokeza.

Tahadhari hiyo imetolewa na Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(TAKUKURU) Frank Mkilanya wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Amesema kuwa kila mwananchi analo jukumu la kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika eneo lake, hivyo mnapobaini utekelezaji mbovu wa miradi mnapaswa kutoa taarifa kwani madhara ya rushwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo yanamgusa kila mwanajamii.

Aidha amesema kuwa taasisi hiyo katika kipindi cha Julai - Septemba 2021 imefanya ukaguzi na ufatiliaji wa utekelezaji wa miradi 12 ya maendeleo yenye thamani ya  bilioni 22.

" Kati ya miradi 12 iliyokaguliwa, miradi 5 inahusu ujenzi wa vituo vya kilimo yenye thamani ya sh.444,775,550, miradi 3 ya elimu yenye thamani ya sh.1,150,000,000,miradi 2 ya idara ya  afya yenye thamani ya sh.215,573,486.45,mradi 1 ujenzi wa soko kuu wenye thamani ya sh.20,739,695,080,maradi 1 ujenzi wa barabara wenye thamani ya sh.158,000,000, Kati ya miradi hiyo miradi 5 imekamilika na 7 inaendelea na hatua mbalimbali za utekelezaji",amesema

Mwishooo

No comments