lemela yafanikiwa kuwapanga machinga 3187 kwenye maeneo rasmi
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Wafanyabiashara wadogo maarufu Kama machinga wapatao 3187 wamepangwa kwenye maeneo rasmi katika Halimashauri ya manispaa ya Ilemela.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa manispaa hiyo Modest Apolinary wakati akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani cha robo ya kwanza cha julai-Septemba cha mwaka wa fedha 2021/2022.
Amesema jumla ya wafanyabiashara wadogo 3187 wakiwamo wanaume 2345 na wanawake 842 wamefanikiwa kupelekwa kwenye masoko rasmi yaliyopo kwenye wilaya hiyo.
" Tumewapeleka kwenye masoko mbalimbali yakiwamo Nyasaka,Kirumba,Buzuruga,Nyamanoro,Pasiansia,Buswelu kitangiri kwani zoezi hili linafanyika sambamba na kuboresha miundo mbinu ya kuweka taa,maji ",amesema Apolinary.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo Hassan Masala amesema yoyote atakaye kutwa kwenye maeneo yasiyo rasmi anafanya biashara watamchukuliwa hatua za kisheria.
Naye Mbunge wa jimbo la Ilemela Dk Angeline Mabula ameishauri halmashauri hiyo kujenga eneo la machinga complex ili kuondoa changamoto ya wafanyabiashara kukosa maeneo.
Naye Diwani wa kata ya Ilemela Willbard Kilenzi amewapongeza Mkurugenzi,Mkuu wa Wilaya kwa kufanya zoezi hilo kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali na kupelekea kufanikiwa bila changamoto yoyote.
Mwishooo.
No comments