Breaking News

WANAWAKE BODI YA MAJI WAWAKUMBUKA WAZEE BUKUMBI

Sarah Onesmo MWANZA, Kuelekea siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika march 8 ya kila mwaka ,Wanawake kutoka bodi ya maji bonde la Ziwa Victoria wamefika katika kituo cha kulea wazee cha Bukumbi Mkoani Mwanza na kupeleka mahitaji kwa wazee hao ikiwa sehemu ya kuadhimisha siku hiyo.
kituo hiki cha kulea wazee wasiojiweza cha Bukumbi kina jumla ya wazee 31 ambaoo kati yao wanaume ni 9 na wanawake ni 21 na mtoto mmoja. Katika kuadhimisha siku ya wanawake dunia ,Wanawake wa bodi ya maji bonde la Ziwa Victoria wamefika katika kituo hiki na kuwashika mkono wazee hawa Kwa kuealetea mahitaji maalum ikiwemo chakula na mavazi.
Akikabidhi vitu hivyo Afisa uhusianao wa bodi hiyo Perpetua Massaga Alisema "Sisi kama wanawake tunatambua mchango wa wazee hawa katika jamiii yetu hivyo hatuwezi kuwasahau ni lazima tuwakumbuke na ndo maana tumekuja kuwaletea zawadi hii kidogo"
Kwa upande wake kaim mkuu wa kituo hicho cha kulea wazee cha Bukumbi Josephine Simba ameshukuru wanawake hao Kwa kuwakumbuka wazee hao na kusema kwamba Kwa Sasa kituo hicho kinakabiliwa na changamoto ya uzio ili kuimarisha ulinzi kwa wazee hao. "Tunaishukuru sana serikali ya awamu ya sita inawakumbuka wazee wetu imeboresha huduma ya afya Kwa wazee hawa na Kwa Sasa wazee wote katika kituo hiki wanakadi za Bima ya afya"Alisema Josephine Simba
Baadhi ya wazee katika kituo hicho akiwemi Charles Mbuguku pamoja na Mariam Ally wamewashukuru wanawake hao wa bodi ya maji bonde la Ziwa Victoria kwa kuwaletea zawadi hizo na kuomba watu wengine wawakumbuke Kwa kwenda kuwapelekea mahitaji mengine.

No comments