Breaking News

Mkifuata Kanuni hizi Mtajikinga na Saratani ya Shingo ya Kizazi.


Na Maridhia Ngemela, Mwanza

Imeelezwa kuwa Saratani ya shingo ya kizazi inaongoza katika aina mbalimbali za ugonjwa huo hapa nchini.

Saratani ni ugonjwa unaosababishwa na kugawanyika kwabseli za kiungo chochote mwilini bila kufuata utaratibu wa kawaida.

Miongoni mwa aina za Saratani ni Saratani ya shingo,Saratani ya Ini,Saratani ya Koo,mapafu,ngozi,Saratani ya ubongo,tumbo,mifupa,kongosho,Macho,Shingonya kizazi, Utumbo mpana,Ulimi, na Damu.

Daktari bingwa wa upasuaji kutoka hospital ya Rufaa ya Mkoa Sekou-Toure Dkt.Athanas Ngambakubi amebainisha kuwa Saratani ya shingo ya kizazi inaongoza kwa wanawake ameyabainisha hayo alipokuwa akitoa mafunzo ya siku Moja  kwa waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza juu ya namna ya kuielimisha jamii kuhusiana na afya za ugonjwa wa Saratani kupitia mradi mtambuka wa Saratani Tanzania (TCCP) kwa ufadhili wa Shirika la maendeleo la Ufarasa (AFD) na Aga Khan foundation (AKF).

Dkt.Ngambakubi amesema kuwa,mwaka 2020 inakadiriwa watu millioni 1.1 walipata Saratani  huku watu 711,429 walifariki kwa Saratani Afrika wakati  Tanzania 49,464 walipata  Saratani na Kati yao 26,945 walifariki  kutokana na ugonjwa huo.

Dkt.Ngambakubi amebainisha kuwa hakuna dalili rasimi ya kugundua ugonjwa huo peke yake hivyo mgonjwa wamagonjwa mengine kama uvimbe ,kuchoka sana,kutapika ,kuharisha,kupunguza uzito,vidonda visivyo pona,kutoka damu ukeni na harufu mbaya.

Ameishauri jamii kuwahi kupatiwa matibabu mara tu wanapohisi dalili zinazoweza kusababisha ugonjwa wa Saratani. 

Amesema kuwa Kuna aina mbili  za  viatarishi vinavyoweza kuongeza uwezekanowa mtu kupata  Saratani ikiwemo vihatarishi visivyoweza kuzuilika.
 
Ameongeza kuwa,viashiria vinavyoweza kuzuilika ni miongoni mwa baadhi ya kuacha tabia ya matumizi ya pombe ,ngono zembe ikiwa ni pamoja na kuacha kutumia vitu vyenye kemikali.

Dkt.ngambakubi amebainisha kuwa,hakuna  kinga ya kuzuia mtu asipate Saratani mtu mwenyewe apunguze uwezekano wakupata kuzingatia chanjo ya Saratani ya Ini na shingo ya kizazi na kuacha matumizi ya tumbaku,pombe, chumvi,na mafuta.

No comments