EMEDO YATAMBULISHA MRADI WA KUZUIA KUZAMA ZIWA VICTORIA ,RAS AWATAKA EMEDO NA WADAU KUISAIDIA SERIKALI
Na Tonny Alphonce,Mwanza
Kutokana
na kuongeza kwa shughuli za kiuchumi katika Ziwa Victoria wadau wametakiwa
kuongeza jitihada za kuzuia ajali za wavuvi kuzama maji kwa manufaa ya mkoa na
taifa kwa ujumla.
Akizungumza
katika utambulisho wa Mradi wa Kuzuia Kuzama Maji Ziwa Victoria unaotekelezwa
na Shirika la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo EMEDO katibu Tawala Mkoa Wa
Mwanza Elikana Balandya amesema mradi huo umekuja wakati pia serikali imeamua
kuwekeza katika Ziwa Victoria hivyo
wadau hawana budi kushirikiana na serikali katika kuhakikisha uwekezaji huo unakuwa
na tija.
“Kwa
sasa Mkoa wetu wa Mwanza Serikali inatekelezeka
mpango wa BBT (Building Better Tomorrow) katika sekta ya ufugaji na uvuvi hivyo
mradi wa kuzuia kuzama maji katika Ziwa Victoria utasaidia kutoa elimu ili
kuzuia vifo zitokanavyo na kuzama maji na wananchi wataweza kufanya shughuli
hizi za uvuvi kwa usalama”.alisema Balandya
Kwa upande wake Arthur Mjema afisa mradi kutoka shirika la EMEDO amesema katika utekelezaji wake mradi utayagusa makundi manne ambayo ni Wavuvi,Watoto,kundi la kina mama wachakataji na kundi la nne kundi la vijana wasomba ngese.
Mgema
amesema lengo hasa la kuyagusa makundio hayo ni kutokana na majibu ya utafiti
ambayo yanaonyesha kuwa makundi hayo manne ndio makundi yaliyopo kwenye hatari
ya kuzama maji.
Mkufunzi
wa Chuo Cha Wanamaji Mwanza ASP Roberth Kelese ambae alipatiwa mafunzo ya
uokoaji nchini Uingereza kupitia mradi huo akawataka wadau kuungana na EMEDO
ili kuhakikisha mradi unafanikiwa.
“Nilipokuwa
Uingereza nimejifunza kuwa janga hili si lakuiachia taasisi moja peke yake
lazima wadau tuungane ili kupambana na ajali hizi za majini ambazo kiukweli
zinapoteza maisha ya watu wengi duniani kote”.alisema ASP Kelese.
No comments