Breaking News

TCAA YAIBUKA MSHINDI WA PILI NA KUPEWA TUZO YA UTENDAJI BORA WIZARA YA UCHUKUZI 2023


Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Hamza Johari tuzo ya mshindi wa pili ya kiutendaji miongoni mwa taasisi chini ya Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka 2023.
Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Hamza Johari akifurahia tuzo ya mshindi wa pili ya kiutendaji miongoni mwa taasisi chini ya Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka 2023 mara baada ya kukabidhiwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Hamza Johari akiwa timu ya maonesho ya TCAA wakifurahia tuzo hiyo.
****

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imeibuka mshindi wa pili na kupokea tuzo ya kiutendaji miongoni mwa taasisi chini ya Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka 2023.

Tuzo hiyo imekabidhiwa na Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa alipokuwa akizindua Mkutano wa 16 wa Tathimini ya Utekelezaji katika Uchukuzi na Usafirishaji jijini Arusha na kupokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Hamza Johari.

No comments