Breaking News

Wafugaji washauliwa kutumia madume ya Ankole na Ng'ombe wa kienyeji kwaajili ya uzalishaji.
Na Hellen Mtereko, Mwanza

Wafugaji wameshauriwa kutumia madume ya Ankole na Ng'ombe wa kienyeji kwaajili ya uzalishaji kwani ni mfumo mzuri utakao wasaidia kuwa na ufugaji wenye tija.

Ushauri huo umetolewa na mtafiti wa mifugo kutuko taasisi ya utafiti wa mifugo Tarili kituo cha Mabuki kilichopo Wilaya ya Misungwi Jijini Mwanza, Godfrey  Chasama wakati wa ziara ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), waandishi wa habari na watafiti, iliyolenga kutembelea miradi mbalimbali inayofadhiliwa Costech.

Alisema kuwa wafugaji wengi bado wanafuga kijadi hali inayopelekea kuona ufugaji wao hauna tija,aliongeza kuwa moja ya shughuli ambazo wamefanya kwa kipindi kirefu chini ya utafiti huo kwenye idara ya Ng'ombe ni kuboresha uwezo wa Ng'ombe kiuzalishaji ambao kiutaalam unaitwa  (BLEEDING).

Chasama alieleza kuwa mwaka 2012 walianzisha utaratibu wa kupanga kitu na wafugaji ambao wanafikika kirahisi katika maeneo ya jirani kulingana na Ng'ombe waliopo(outreach program) ambayo ililenga kuboresha Ng'ombe wa Zibu aina za Kisukuma na Tarime kwakutumia aina ya Ankole ambae kiuzalishaji ana ubora mkubwa ukilinganisha na Zibu.

James manjara mfugaji anae simamia mifugo ya Baba yake Michael Lusomi akiwa

Alisema kuwa wanafanya kazi ya kuzalisha mbegu kwakufanya tathimini ya wanyama tangu anapozaliwa anachukuliwa uzito,anapoachishwa kunyonya anachukuliwa uzito na anapotimiza mwaka mmoja anachukuliwa uzito,mwisho wanaangalia vigezo vya kuwachagua ambao wako kwenye asilimia 60 wanakuwa na ubora wa kusambazwa Kama mbegu kwa wafugaji ambao wanahusishwa kwenye outreach program.

"Matokeo ya ufugaji yalikuwa ni mazuri kwani Ng'ombe walikuwa wanazaliwa na wanakuwa vizuri na mfugaji anatafutwa sana na wanunuaji wa Ng'ombe na hata akienda mnadani anakuwa na uhakika wa kuuza",alisema Chasama

Kwaupande wake Mtoto wa Michael Lusomi anaesimamia shughuli zote za ufugaji wa Ng'ombe James Manjara alisema kuwa walianza ufugaji wa mchanganyiko baada ya kupewa elimu na watafiti kutoka Taasisi ya Taliri.

"Tulipewa elimu ya ufugaji wa kutumia mfumo wa madume ya Ankole na Ng'ombe wa kienyeji,tulianza ufugaji huo wa mchanganyiko ambao umetuletea mabadiliko makubwa sana ukilinganisha na ufugaji wa zamani",alisema Manjara

Alisema kuwa pamoja na changamoto wanazopitia ikiwemo magojwa na malisho bado wanajitahidi sana kukabiliana nazo ili kuweza kuwakomboa.


Wakwanza (kulia) ni mtafiti wa mifugo kutuko taasisi ya utafiti wa mifugo Taliri Godfrey Chasama akiwa na James manjara ambae ni mfugaji

Manjara aliongeza kuwa mwanzoni walikuwa wakiuza Ng'ombe wa kienyeji wa miaka 2 kwa laki 2 lakini kwa sasa Ng'ombe wa miaka miwili wanauza laki 5  hadi 7 hivyo utofauti ni mkubwa sana Kati ya Ng'ombe wa kienyeji na hawa wa mchanganyiko.

Alieleza kuwa kwaupande wa maziwa pia kunautofauti mkubwa kwani Ng'ombe mmoja wa mchanganyiko ukimkamua unapata lita moja na nusu au mbili za maziwa lakini wa kienyeji  walikuwa wanapata robo lita.

Mwisho alitoa wito kwa wafugaji wengine ambao hawajaanza ufugaji wa mchanganyiko wajitokeze wapate elimu ili waweze kufuga ufugaji  huo wenye tija  utakaoweza kuwatimizia mahitaji yao Kama ilivyo kwao inavyowasaidia katika shida mbalimbali ikiwemo kulipa ada.

Mwishoo

No comments