Wananchi waombwa kujitokeza kupima magonjwa mbalimbali ikiwemo figo..
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Wananchi Mkoani Mwanza wameombwa kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya furahisha kwaajili yakupima vipimo mbalimbali ili waweze kubaini magonjwa yanayowakabili
Akizungumza katika maadhimisho ya sherehe ya miaka 50 ya hosptali ya Kanda Bugando, Mkurugenzi wa huduma za tiba katika hosptali hiyo Dk Bahati Wajanga amesema kuwa Wananchi watumie fursa hiyo ili waweze kujua afya zao hali itakayowasaidia kuchukua hatua sitahiki ikiwa ni pamoja na kupata ushauri, matibabu.
Amesema kuwa Wananchi wakijitokeza kwa wingi itakuwa ni nafasi nzuri kwa wataalamu kuweza kubaini ni magonjwa gani yanayowakabili wakazi wa Jiji la Mwanza.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa kamati ya kuratibu maadhimisho ya miaka 50 ya hosptali ya Bugando profesa William Mahalu ambae pia ni daktari bingwa mbobezi wa upasuaji wa moyo na vifua, amesema kuwa kwa hapa Mwanza madaktari bingwa wapo katika viwanja vya furahisha hivyo wananchi wafike kwaajili yakupatiwa huduma.
Amesema hosptali hiyo kwa sasa inajivunia kuwa na kipimo Cha juu zaidi(MRI) ambacho wamekipata hivi karibuni .
Mahalu ameeleza kuwa katika sherehe hizo za miaka 50 wamekuwa wakitoa huduma mbalimbali za matibabu kwa wananchi kwenye Mikoa ya Geita,shinyanga, Mara na Simiyu na kwa hiyo Mikoa walihudumia wagonjwa 1896 na walifanya oparesheni 240.
Awali akizungumza katika maadhimisho hayo Mkurugenzi wa hospital ya Kanda Bugando dk Fabian Masaga amesema lengo la maadhimisho hayo ni kuendelea kutoa huduma kwa wananchi wenye magonjwa mbalimbali ili waweze kuwa na uhakika wa afya zao.
Amesema magonjwa huchangia sana katika kushusha uchumi wa mtu mmoja mmoja,jamii na Taifa kwa ujumla hivyo wananchi wawe na utaratibu wa kufanya chekapu waweze kubaini magonjwa ili wafanye kazi zao za kujiingizia kipato wakiwa na afya njema.
Mwishoooo
No comments