Breaking News

MSAFARA WA MAGUFULI WAVUKA KIGOGO - BUSISI,SIMANZI YATAWALA WAINGIA GEITA

 


Na Tonny Alphonce,Mwanza


 

Msafara wa viongozi na mwili wa aliyekuwa Rais wa tano Hayati Dkt.John Magufuli umevuka katika kivuko cha Kigongo - Busisi  mara tu baada ya wananchi wa Mwanza kupata nafasi ya kutoa heshima za mwisho.

Katika msafara huo wananchi wameonekana wakiwa na huzuni na simanzi huku wakiwa wamesimama pembezoni mwa barabara na kutoa heshima zao za mwisho kwa Hayati Dkt John Pombe Magufuli.
Mapema leo asubuhi, wananchi wa mkoa wa Mwanza na mikoa ya jirani walijitokeza kuupokea mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa ndege wa Mwanza na baadae katika uwanja wa CCM Kirumba na kutoa heshimazao za mwisho.Hayati Dkt. Magufuli alifariki dunia Jumatano Machi 17, 2021 katika hospitali ya Mzena, Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu na anatarajiwa kuzikwa Ijumaa Machi 26 wilayani Chato mkoani Geita.

 

No comments