Breaking News

SERIKALI YAAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO ZA WANAHABARI.

                     Klabu ya Waandishi Mkoa wa Mwanza (MPC) ikishirikiana na Taasisi ya Kihabari ya Internews.
Tarehe 19.08.2021 imefanya mkutano wa tathimini ya mwenendo wa vyombo vya Habari Kwa robo ya pili ya mwaka 2021.

Mgeni Rasmi katika mkutano huo uliofanyika kwa njia Zoom, Bw. Rodney Thadeus Mkurugenzi msaidizi wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo alielezea Kwa kina nia ya serikali kujikita katika kuvifungulia vyombo vya habari vilivyofungiwa pia aliwataka waandishi kufanya kazi kwa weledi ili kuepuka vyombo vyao kufungiwa.

Bwana Rodney pia alisema kuwa, Serikali imepokea changamoto zote za wanahabari Nchini na itahakikisha inaweka mikakati ya kuzitatua.

Pia aliwataka waandishi wa habari kuwa huru kwenye kusema vikwazo vinavyokwamisha utendaji wa shughuli zao.

Kwa upande wake mwakilishi toka Shirika la Internews Shaban Maganga alisema kuwa, waandishi wa habari ni kundi muhimu kwenye kuleta mabadiliko ya Taifa hivyo lazima lijisimamie.

Katika mkutano huo mada mbalimbali ziliwasilishwa na baadaye kuwa na majadiliano ya pamoja ambapo baadhi ya wanahabari waliitaka serikali kuangalia sheria na kanuni zinazowanyima uhuru waandishi zifanyiwe marekebisho


No comments