Breaking News

Wanahabari Kanda ya ziwa Wapata mafunzo ya Sheria

 

Chama cha wanasheria wa Afrika masharika chini ya mkurugenzi Mtendaji  Wakili  David Sigano kwa kushirikiana na  baraza la habari Tanzania (MCT) wameandaa  mafunzo kwa waandishi wa habari, ambapo Mafunzo haya yamefanyikia jijini Mwanza.


Mwenyeji wa mafunzo haya akiwa ni Klabu ya waandishi wa Habari wa mkoa wa Mwanza (MPC)  chini ya Mwenyekiti wake Ndugu Edwin Soko. 


Mafunzo haya yakiwa na lengo la kuangalia changamoto na  mwenendo katika suala la uhuru wa kujieleza, uhuru wa vyombo vya habari, hali ya kupata taarifa na kufanya kazi katika ufanisi kwa waandishi wa habari, sambamba na majadiliano juu ya sheria za vyombo vya habari.


Picha Mbalimbali za washiriki katika semina hiyo ya siku moja.
No comments