Breaking News

MFUKO WA MAWASILIANO KWA WOTE (UCSAF) KUJENGA MINARA YA KURUSHIA MATANGAZO YA RADIO NCHI NZIMA

 

Na Tonny Alphonce,Mwanza


Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa (UCSAF) na wadau wenye Leseni za huduma za mawasiliano Kanda ya Ziwa.

Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) umesema unatarajia kujenga minara ya kurushia matangazo ya Radio kwa nchi nzima ili kuwapunguzia wamiliki wa Radio gharama za kukodi minara kutoka kwa watu binafsi.

Afisa sheria mwandamizi wa UCSAF Bwana Fredy Kandonga .

Akizungumza na Wadau wenye Leseni za huduma za mawasiliano Kanda ya Ziwa,afisa sheria mwandamizi wa UCSAF Bwana Fredy Kandonga amesema katika ujenzi huo wa minara nchi nzima,watashirikiana na halmashauri pamoja na TCRA ambapo wamiliki wa Radio watakaotumia minara hiyo watalipa pesa za uendeshaji wa minara hiyo.

'Mwanzoni tumejenga minara mingi ya simu katika maeneo ambayo hayakuwa na huduma hiyo lakini awamu hii baada ya maombi ya wadau tunakuja na mradi huu mkubwa wa ujenzi wa minara ya kurushia mawimbi ya radio kwa nchi nzima,alisema Kandonga.'

Awali Akifungua Mkutano wa wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa leo Jumanne Februari 15,2022 Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) amewataka watoa huduma za mawasiliano kushirikiana na kuacha kubaguana.


    Waandishi mmekuwa na tatizo kubwa la kubaguana na kusemana vibaya,acheni tabia hiyo na muungane mtafika mbali,hata hili la minara mkiungana linawezekana kabisa alisema Mhandisi Francis 

Aidha amehamasisha watoa huduma za mawasiliano kwa njia ya redio kuongeza usikivu akibainisha kuwa nafasi za kuongeza usikivu wa Redio kwenye maeneo mbalimbali zipo na TCRA inaendelea kuzitoa.


Wadau wa huduma za mawasiliano Kanda ya Ziwa, wakifatilia wasilisho la afisa sheria mwandamizi wa UCSAF Fredy Kandonga hayupo pichani.


Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwa kwenye mkutano ulioandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF).


Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwa kwenye mkutano ulioandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF).

Credit: (PICHA) Malunde Blog.




No comments