Breaking News

SHIRIKA LA TMFD NA MYCN WAINGIA MAKUBALIANO YA KIMKAKATI KWENYE KUFANYA KAZI KWA PAMOJA

 

Na Mwandishi wetu - Mwanza.

Shirika la Tanzania Media for Maritime and Fisheries Development (TMFD) leo April 5, 2023 limeingia kwenye makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja na shirika la Mwanza Youth and Children Network (MYCN) katika maeneo ya  jinsia, haki za binadamu, afya na uezeshwaji wa jamii.

Mkurugenzi wa TMFD Bwana Edwin Soko amesema kuwa, hatua hiyo ni hatua muhimu kwa kuwa TMFD inafanya kazi nyingi zinazoendana na shughuli zinazotekelezwa na MYCN hivyo makubaliano hayo yataongeza nguvu ya utendaji na utafutaji wa matokeo bora ya miradi.
Naye Mwenyekiti mtendaji wa shirika la MYCN Bwana Brightius Titus amesema kuwa, makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja yataleta ufanisi kwenye kutekeza vyema malengo ya mipango iliyowekwa kwa mashirika yote mawili na kupunguza changamoto za watoto na vijana.

Moja ya makubaliano hayo ni kutafuta miradi kwa pamoja, kutekeleza miradi, kufanya tathimini ya miradi na kutoa taarifa ya miradi kwa pamoja.

Makubaliano hayo yamefanyika kwenye ofisi za MYCN zilizopo Jijini Mwanza.

No comments