Video : 8th WONDER - FINALLY
Ni msanii Mashuhuri wa muziki akiwa anawakilisha nchini Nigeria akiwa mbobezi katika muziki asilia zaidi na kuendelea kuonyesha zaidi tamaduni za muziki wa Kinaijeria .
Licha ya kufanya muziki pia 8th Wonder amekuwa akitumia zaidi nafasi yake kusaidia kuchangisha fedha kwa ajili ya elimu ,afya na umaskini nchini Nigeria.
Amefanikiwa kufanya kazi tofauti tofauti lakini kwa sasa ameachia rasmi kazi yake mpya iitwayo “Finally” ikiwa audio imetayarishwa na mtayarishaji mashuhuri kutoka nchini Nigeria Masterkrafts.
Sanjari na video ya wimbo huo ikiwa imeongozwa na WG Films ikiwa imefanyikia katika maeneo mbali mbali jijini Lagos Nigeria.
8th Wonder ni msanii ambaye anafanya kazi chini ya Lebo ya muziki ya IJ.
Finally ni wimbo ambao kwa sasa unapatikana katika vyanzo vyote vya kupakua na kusikiliza muziki na vile vile unaweza kumfatilia katika mitandao yake ya kijamii @wonderthahypeman ili kuwa karibu zaidi na kazi zake.
Tazama Video hapa chini
No comments