Breaking News

PICHA; TIMU YA MTOTO KWANZA MWANZA YAJITAMBULISHA KWA RAS

 Na Tonny Alphonce,Mwanza



Timu ya Mtoto Kwanza inayotekeleza  Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM)2021/22-2025/2026 kwa mkoa wa Mwanza imejitambulisha rasimi kwa katibu Tawala wa mkoa huo Elikana Balandya.

 Akizungumzia program hiyo kwa  kifupi mbele ya RAS, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mwanza Janeth Shishila amesema program hii inawalenga watoto wenye umri wa miaka 0-8 ambao wanahitajika kuangaliwa kwa ukaribu na kufanyiwa uwekezaji ili waweze kuwa rasilimali bora kwa familia na taifa kwa ujumla.

Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mwanza Janeth Shishila akielezea namna programu ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto itakavyolinufaisha Taifa.

Nae mratibu wa miradi ya elimu kutoka shirika TAHEA Bwana Peter Matyoko amesema program hii itagusa maeneo matano muhimu kwa mtoto ambayo ni Afya,Lishe,Malezi yenye Mwitikio,Ujifunzaji wa Awali na Ulinzi na Usalama wa Mtoto.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa mkoa  wa Mwanza Elikana Balandya amesema mkoa upo tayari kupokea program hiyo na mkoa unatambua umuhimu wa kuwekeza kwa watoto hasa wa umri huu wa 0-8 na kuongeza kuwa hivi sasa mkoa unakikisha kila shule ya msingi inayojengwa ina kuwa na darasa la awali.


 Katibu Tawala wa mkoa  wa Mwanza Elikana Balandya akisikiliza kwa makini namna programu ya Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto itakavyomsaidia mtoto wa Kitanzania.

Mazungumzo yakiendelea.

No comments