Breaking News

MSEMAJI WA JESHI LA POLISI AWATAKA WAANDISHI WA HABARI KUWA MSTARI WA MBELE KULINDA MASLAI YA TAIFA

 

SACP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi akizungumza na waandishi wa habari katika mdahalo wa kitaifa wa ulinzi na usalama wa mwandishi wa habari, uliaondaliwa na UTPC Jijini Dodoma.

Umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) imefanya mdahalo wa kitaifa wa ulinzi na usalama wa mwandishi wa habari, mdahalo huo umefunguliwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini David Misime, ambapo amewataka waandishi wa habari kuwa mstari wa mbele katika kulinda na kukuza maslai ya Taifa wanapotelekeleza majukumu Yao.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa UTPC Kenneth Simbaya juu ya kauli mbiu ya mdahalo huo Inayosema“Shambulio lolote kwa mwandishi wa habari ni Shambulio la Umma”
Kenneth amewataka waandishi wa habari kufanya kazi zao kwenye mazingira rafiki bila kubuguziwa, na kufanya kazi bila hofu ili waweze kupata taarifa sahihi na kutoa taarifa sahihi kwa jamii.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tamwa Dkt. Rose Reuben amesema asilimia 64 ya wanawake walipo katika Vyombo vya habari vya Jiji la Dar es Salaam wamefanyiwa unyanyasaji wa kingono, na changamoto kubwa zinazojitokeza ni waandishi hao wanashindwa kuripoti kwa sababu ya kukosa fursa za kikazi.
No comments