Breaking News

NIC YAWATAKA WANANCHI KUKATA BIMA ILI KUJIKINGA NA MAJANGA YANAYOTARAJIWA KUIKUMBA NCHI

 

Na Tonny Alphonce,Mwanza

Wananchi wameombwa kukata bima za nyumba ili waweze kulinda nyumba zao na mvua kubwa za Elinino zilizotabiria kuanza kunyesha hapa nchini mwaka huu 2023.


Kauli hiyo imetolewa na meneja wa shirika la Bima kanda ya ziwa (NIC) Stela Marwa wakati akizungumza na waandishi wa habari waliofika katika ofisi hizo ili kujua shunghuli mbalimbali zinazofanywa na NIC pamoja na kuzungumzia Usiku wa wadau wa habari kanda ya ziwa utakaofanyika tarehe 20/10/2023.

Stela amesema ni vema wananchi wanaomiliki nyumba wakakata bima za nyumba  ili waweze kujikinga majanga yasiyoweza kuzuilika kama vile mafuriko au ikiungua moto ili waweze kulipwa fidia kupitia bima za nyumba.

Meneja wa shirika la bima kanda ya ziwa (NIC) Stela Marwa wakati akizungumza na waandishi wa habari hawapo kwenye picha.

"Wote tunasikia kupitia vyombo vya habari kuwa kuna mvua kubwa zitanyesha hapa nchini sasa niwashauri wananchi mkate bima ya nyumba hii italinda nyumba na majanga kwa hiyo niwaombe wananchi tusipuuze wataalamu wa utabiri wa hali ya hewa maana wamesema kuna hizo mvua kubwa na zinaweza kuleta madhara sisi NIC tupo tayari kuwalipa fidia".alisema Stela

Stela amewataka pia waandishi wa habari kukata bima ya Personal Accident ili iweze kuwalinda wanapokuwa kazini au nje ya kazi endapo mwandishi wa habari  akipata ajali au kupingwa akiwa katika majukumu yake atafidiwa na bima hii.

Akizungumzia usiku wa Wadau wa Habari Kanda ya Ziwa,Stela amekipongeza chama cha waandishi wa habari mkoa (MPC) kwa kuandaa usiku huo utakaowakutanisha wadau wa habari kwa lengo la kufahamiana na kubadilishana mawazo.

No comments