Breaking News

WALIMU WA WALEZI SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI NA VYUO SHINYANGA WAPATIWA MAFUNZO UANZISHWAJI WA KLABU ZA MAADILI

 
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Ibrahim Makana akizungumza wakati akifungua mafunzo kuhusu uanzishwaji wa Klabu za Maadili kwa Walimu wa Malezi wa Klabu za Maadili shule za msingi, sekondari na vyuo katika Mkoa wa Shinyanga.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Ibrahim Makana akizungumza wakati akifungua mafunzo kuhusu uanzishwaji wa Klabu za Maadili kwa Walimu wa Malezi wa Klabu za Maadili shule za msingi, sekondari na vyuo katika Mkoa wa Shinyanga.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi imetoa mafunzo kuhusu uanzishwaji wa Klabu za Maadili kwa Walimu wa Malezi wa Klabu za Maadili shule za msingi, sekondari na vyuo katika Mkoa wa Shinyanga.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo leo Jumatatu Oktoba 23,2023, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Ibrahim Makana amesema lengo la Klabu za Maadili ni kuwajengea wanafunzi na wanavyuo misingi bora ya maadili tangu wakiwa shuleni au vyuoni.

Amesema Klabu za maadili za wanafunzi ni vikundi vya wanafunzi ndani ya shule au vyuo nyenye jukumu la kuratibu na kufanikisha shughuli za kuelimisha, kuhamasisha na kushirikisha jamii masuala ya maadili na kwamba Klabu hizo zinalenga kuimarisha nidhamu na uzalendo kwa Watanzania.

“Klabu za maadili kwa wanafunzi zina kazi kubwa ya kuelimisha wanafunzi wengine na wananchi kuhusu maadili kupitia nyimbo, kwaya, maigizo, ngonjera, katuni shairi, ngoma na ubunifu mwingine wowote kwa lengo la kujenga tabia njema na kukemea vitendo vya tabia zisizokubalika katika jamii yetu",amesema.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Ibrahim MakanaAidha kutokana na umuhimu wa klabu hizo za Maadili katika kukuza maadili ya Watanzania, amezielekeza shule na vyuo vyote Mkoa wa Shinyanga kuanzisha Klabu za Maadili za wanafunzi na wanachuo ili kuwe na wanafunzi waadilifu. 

“Pia Mratibu wa Maadili Mkoa wa Shinyanga unatakiwa kufanya ufuatiliaji wa klabu hizo ngazi ya shule na vyuo ili kuona zinafanya kazi kama ilivyokusudiwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya wanafunzi wenye maadili mema na kuongeza ufaulu katika masomo yao”,ameongeza.

Aidha, ameshauri ofisi ya Kanda ya Maadili kutoa mafunzo kila inapoona inafaa kwa lengo la kuimarisha uwezo wa walimu kusimamia klabu hizo ngazi ya shule na vyuo, kwa kufanya hivyo itasaidia kuwaandaa wanafunzi kuwa raia wema, viongozi bora na wazalendo kwa Taifa.

Katika hatua nyingine amemshukuru Gerald Mwaitebele kutoka ofisi ya Maadili Kanda ya Magharibi kwa niaba ya Kamishna wa Maadili kwa kuamua Mkoa wa Shinyanga uwe Mkoa wa mfano katika kuanzisha klabu za Maadili ngazi ya shule na vyuo huku akiishukuru Ofisi ya Maadili kwa kusimamia na kukuza maadili ya viongozi wa umma pia kwa kuanzisha klabu za Maadili katika ngazi ya shule na vyuo.

“Klabu hizi zitasaidia kuwajengea wanafunzi uwezo kujua maadili yanayopaswa kuzingatiwa katika ujenzi wa Taifa letu”,amesema

Katibu Msaidizi, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi (Tabora, Kigoma, Shinyanga Simiyu), Gelard Mwaitebele.

Katibu Msaidizi, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi (Tabora, Kigoma, Shinyanga Simiyu), Gelard Mwaitebele amewataka walimu kutumia vikao vya wazazi shuleni kufikisha ujumbe wa masuala ya maadili kupitia Klabu za maadili.

“Tumeamua kuanzisha Klabu za maadili kwa wanafunzi ili kuandaa kizazi chenye maadili ili tuwe na taifa bora, tunataka taifa lenye watu wenye maadili ili tuwe na viongozi waadilifu. Tatizo la maadili lipo katika jamii, walimu ingieni kazini. Msiwe na uoga wa kusimamia maadili serikali ipo kazini, Mama, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan yupo kazini”, amesema Mwaitebele.

Amezitaja sifa za mwalimu wa malezi kuwa ni pamoja na kuwa mwadilifu, mwaminifu, muwazi, mzalendo, mwajibikaji, anayejali, anayethamini utu na mwenye mafanikio katika kazi zake na anayekubalika kimaadili na wanafunzi.

Kwa upande wake, Afisa Maadili Kanda ya Magharibi, Onesmo Msalangi ametaka Klabu hizo zisaidie kulinda maadili katika nchi huku akisisitiza kuwe na ukaribu mkubwa kwa watoto hasa katika kipindi hiki ambacho mambo ya hovyo ni mengi.

“Wafundisheni watoto jinsi kusaidia kazi wazazi. Kuweni makini na hizi TV na simu za mkononi. Kwenye mitandao ya kijamii kuna mema na mabaya, watoto wanaharibika kwa kupewa simu bila uangalizi, tunaharibu kizazi sisi wenyewe, tuwe makini sana na hivi vitu”,amesema Msalangi.
Walimu wa Malezi wa Klabu za Maadili shule za msingi, sekondari na vyuo wakifuatilia mafunzo

“Wafundisheni watoto jinsi ya kutoa taarifa kwa siri ili kudhibiti vitendo viovu shuleni, vyuoni ili kutambua maovu yanayotokea shuleni. Walimu hakikisheni pia mnashawishi wanafunzi wengi zaidi wajiunge kwenye klabu za maadili”,ameongeza Msalangi.

Mratibu wa Klabu za Maadili Mkoa wa Shinyanga, Bakari Kasinyo amesema chanzo kikubwa cha ukosefu wa maadili inaanzia kwa watu wazima na kwamba kuanzishwa kwa Klabu hizo kunaweza kuibadilisha jamii.

Nao waalimu hao wa malezi wameomba ushirikiano kutoka kwa wazazi kwani kuporomoka kwa maadili ya watoto wakati mwingine yanachangiwa na wazazi kwa kuwaruhusu watoto kujifunza mambo machaf.

Aidha wameipongeza na kuishukuru serikali kuanzisha klabu za maadili hivyo watawaeleza wanafunzi namna ya kuwa na maadili na kuwa wazalend katika nchi na namna ya kutetea nchi yao.


MAADILI NI NINI?
Maadili ni mwenendo mwema au namna ya kuishi. Kwa tafsiri rahisi, maadili ni viwango vilivyoanishwa kwa kubaini jambo sahihi na jambo lisilo sahihi ambavyo vinapaswa kuzingatiwa na wanajamii.

Maadili yanajumuisha viwango vya tabia/mila/desturi zilizo njema na ambazo zinakubalika katika jamii.
Katibu Msaidizi, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi (Tabora, Kigoma, Shinyanga Simiyu), Gelard Mwaitebele akizungumza wakati wa mafunzo kuhusu uanzishwaji wa Klabu za Maadili kwa Walimu wa Malezi wa Klabu za Maadili shule za msingi, sekondari na vyuo katika Mkoa wa Shinyanga.
Katibu Msaidizi, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi (Tabora, Kigoma, Shinyanga Simiyu), Gelard Mwaitebele akizungumza wakati wa mafunzo kuhusu uanzishwaji wa Klabu za Maadili kwa Walimu wa Malezi wa Klabu za Maadili shule za msingi, sekondari na vyuo katika Mkoa wa Shinyanga.

Mratibu wa Klabu za Maadili Mkoa wa Shinyanga, Bakari Kasinyo akitoa mada ya uzalendo wakati wa mafunzo kuhusu uanzishwaji wa Klabu za Maadili kwa Walimu wa Malezi wa Klabu za Maadili shule za msingi, sekondari na vyuo katika Mkoa wa Shinyanga.

Afisa Maadili Kanda ya Magharibi, Onesmo Msalangi  akitoa mada kuhusu Mwongozo wa Klabu za Maadili wakati wa mafunzo kuhusu uanzishwaji wa Klabu za Maadili kwa Walimu wa Malezi wa Klabu za Maadili shule za msingi, sekondari na vyuo katika Mkoa wa Shinyanga.
Walimu wa Malezi wa Klabu za Maadili shule za msingi, sekondari na vyuo wakifuatilia mafunzo
Walimu wa Malezi wa Klabu za Maadili shule za msingi, sekondari na vyuo wakifuatilia mafunzo
Walimu wa Malezi wa Klabu za Maadili shule za msingi, sekondari na vyuo wakifuatilia mafunzo
Walimu wa Malezi wa Klabu za Maadili shule za msingi, sekondari na vyuo wakifuatilia mafunzo
Washiriki wa mafunzo kuhusu uanzishwaji wa Klabu za Maadili kwa Walimu wa Malezi wa Klabu za Maadili shule za msingi, sekondari na vyuo katika Mkoa wa Shinyanga wakipiga picha ya kumbukumbu.

No comments