Breaking News

DC ACHARUKA KUCHELEWA UJENZI WA ZAHANATI YA MKOLANI MWANZA

 









Na Mwandishi wetu, Mwanza

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe.Amina Makilagi ametoa siku 6  kwa wasimamizi wa Ujenzi wa Zahanati ya Mkolani kuhakikisha wanakamilisha majengo ya OPD, Jengo la Afya ya Mama na Mtoto ili huduma zianze mara Moja.

Mhe.Makilagi ametoa maagizo hayo alipokuwa kuwa akikagua ujenzi wa miundombinu ya Afya, Elimu, Upandaji Miti ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake wilayani humo.

"Haiwezekani pesa mnazo kwenye account yenu lakini majengo hayakamilliki na sababu hazieleweki,ikifika Novemba 15 Mwaka huu naomba tutakabidhiwe majengo tayari kwa taratibu zingine kufuata",amesema Makilagi 

Mhe. Amina Makilagi akiwa ziarani hapo pia akishiriki upandaji Miti kuzunguka Taasisi hiyo ikiwa ni kampeni yake ya kuhakikisha wanapanda Miti 1.5 Milioni inapandwa maeneo mbalimbali ili kupunguza athari za uchafuzi wa mazingira.





No comments