Breaking News

KUELEKEA SIKU YA KILELE CHA MAONYESHO YA MADINI BANDA LA NBC LAZIDI KUWA KIVUTIO.

Mkuu wa mkoa wa Geita Rosemary Senyamule na Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Amina Mkilagi jana (19/09/20121) wametembelea banda la NBC na kuwapongeza kwa huduma nzuri wanazozitoa kwa wananchi.


Wakiwa katika banda hilo la NBC walipokelewa na wafanyakazi wa benki hiyo ambapo Meneja Maendeleo ya Biashara tawi la Geita, Ally Idd alielezea huduma zinazopatikana katika banda hilo ikiwemo huduma ya kufungua akaunti chap chap pamoja na huduma ya kuweka na kutoa pesa.


Maonyesho ya Nne ya Madini ya Dhahabu yanaendelea mkoani Geita ambapo maonyesho hayo yanatarajiwa kuzinduliwa rasimi tarehe 22/09/2021 na waziri mkuu wa Tanzania Mh Majaliwa Kasim Mjaliwa.


Na Tonny Alphonce,Geita.

No comments