Breaking News

Vijana changamkieni fursa ya michezo mpate ajira


Na Hellen Mtereko, Mwanza

Vijana wameshauriwa kuthamini michezo kwakuwa kwa Sasa michezo imekuwa Ni ajira ya kudumu ambayo inaweza kubadilisha maisha yao.

Ushauri huo umetolewa na Naibu Waziri wa Aridhi Nyumba na maendeleo ya Makazi ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Angelina Mabula wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye hitimisho la mashindano ya Angelina Jimbo Cup 2021.

"Michezo ni mizuri Sana kwani itakufanya uimarishe afya yako na kuepukana na magonjwa nyemelezi,pia ni ajira ya uhakika kwa Vijana sio Tanzania bali hata katika mataifa yote ulimwenguni.

Katika mashindano hayo timu ya Kata ya Kirumba wamefanikiwa kuwa mabingwa wa Mashindano ya Angelina Jimbo Cup 2021,  Baada ya kuifunga timu ya Kata ya Ibungilo kwa jumla ya mikwaju 4-3 ya penati katika uwanja wa CCM Kirumba.


Angelina Mabula Naibu Waziri wa aridh Nyumba na maendeleo ya makazi (Mb) akizungumza na baadhi ya Vijana siku ya hitimisho la mashindano ya Angelina Jimbo Cup 2021 katika viwanja vya CCM Kirumba

 Katika michuano hiyo timu za pande zote zilionekana kuwa na hali na morari ya mchezo ambapo mpaka dakika tisini za mchezo huo kumalizika timu ya Ibungilo na Kirumba zilitoka sare ya kufungana bao 1-1 na ndipo mwamuzi wa mchezo huo aliamuru kupigwa kwa mikwaju ya penati na timu ya kirumba ikaibuka kidedea kwa na kuifanya timu ya Ibungilo kushindwa kutetea ubingwa wake msimu huu.

Mashindano hayo pia yaliambatana na zawadi mbalimbali ambapo timu ya Kirumba iliondoka na zawadi ya shilingi Milioni mbili,seti moja ya jezi na mpira, Mshindi wa pili Ibungilo aliondoka na pesa taslimu shilingi Milioni moja na nusu, seti moja ya jezi na mpira huku mshindi wa tatu Shibula aliondoka na shilingi Milioni moja, seti moja ya jezi na mpira huku zawadi ya Mwandishi bora wa habari za mashindano hayo ilikwenda kwa Alexander  Sanga, mwandishi wa gazeti la Habari leo ambapo ameondoka na kitita cha shilingi laki mbili.

Viongozi mbalimbali waliohudhuria kwenye mashindano ya Angelina Jimbo Cup wakiwa jukwaani.

Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa(NEC) kutoka Wilaya ya Nyamagana Jamal Babu alisema kuwa Vijana ni nguvu kazi ya Taifa hivyo wajikite Sana katika michezo ili waweze kutimiza ndoto zao 

" namshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassani kwajitihada anazozifanya za kuwezesha fedha ili viwanja vya michezo viweze kuboresha, hivyo Vijana tumieni fursa hiyo ili muweze kujikwamua kiuchumi kwani michezo Sasa ni ajira",alisema Jamal


No comments