Breaking News

KIKUNDI CHA WATOTO WANAOISHI NA VVU CHATEMBELEWA NA NACOPHA.

Na Tonny Alphonce,Mwanza

Kikundi cha watoto wanaoishi na Virusi vya UKIMWI cha Wisdom kilichopo Nyamagana Mkoani Mwanza kimelishukuru Baraza la Watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA) kanda ya Mwanza kwa kukitembelea kikundi hicho na kuwapa moyo katika jitihada zao za kutoa elimu ya Virusi na UKIMWI.

Kwa mujibu wa katibu wa Konga ya Nyamagana,Joseph Kialacha amesema kikundi hicho hadi sasa kina watoto 16 na kinaendelea kukua siku hadi siku japo wamekuwa wakikutana na baadhi ya vikwazo kutoka kwa wazazi na walezi.

Akizungumza na wanakikundi hao mratibu wa mradi wa Hebu Tuyajenge Bi Veronica Joseph amewasisitiza watoto kuzingatia matumizi ya dawa na kuendelea kutoa elimu kwa watoto wengine wenye VVU waweze kujiunga na kikundi hicho.

                   Picha ya pamoja wanakikundi wa Wisdom na Wafanyakazi wa NACOPHA Mwanza.


Mwenyekiti wa kikindi cha Wisdom Sadu Yusuph akipokea zawadi kutoka kwa mratibu wa mradi wa Hebu Tuyajenge Bi Veronica Joseph.

Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Sawa,Dkt Herman Yohana akipokea zawadi kutoka kwa mratibu wa mradi wa Hebu Tuyajenge Bi Veronica Joseph ikiwa ni sehemu ya shukrani kwa kuwahudumia watoto wa kikundi cha Wisdom.

Viongozi wa NACOPHA wakifurahia jambo wakati walipokitembelea kikundi cha watoto cha Wisdom.
No comments