Wakulima watakiwa kukata bima
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Wakulima wa Kanda ya Ziwa wametakiwa kukata bima za kilimo ili waweze kukabiliana na majanga mbalimbali yatokanayo na shughuli za kilimo kwa lengo la kujihakikishia usalama wa mazao yao.
wito huo umetolewa na meneja wa Mamlaka ya usimamizi wa bima(Tira) Kanda ya ziwa, Sharif Hamadi wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya umuhimu wa wakulima kuwa na bima za kilimo.
Alisema kuwa kwa sasa Kuna mashirika yanayoto huduma za bima za kilimo hivyo ni wakati Sasa wakulima kujiunga na bima za kilimo kwaajili ya manufaa yao.
Hamad alisema kuwa sekta ya kilimo imekuwa na mchango mkubwa Sana kwaajili ya maendeleo ya kilimo,na imekuwa ikichangia pato la Taifa hivyo ni mihimu kwa wakulima kujihakikishia usalama wa mazao yao kwa kukata bima za kilimo.
Meneja wa Mamlaka ya bima Kanda ya ziwa Sharif Hamad akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake
"Kuna kampuni za bima ambazo zinatoa huduma za bima za kilimo, hivyo wakulima changamkieni fursa ili muweze kupata fidia ya mazao yenu pindi majanga yanapowakuta yakiwemo mafuriko yanapowakumba",alisema Hamad
Aliongeza kuwa kilimo kina mchango mkubwa katika maendeleo ya sekta ya viwanda Nchini na kuwa wakulima ni lazima waendeshe shughuli za kilimo kwa manufaa kutokana na kuwa na bima za kilimo kwa ajili ya mazao yao
Aliyataja baadhi ya majanga ambayo wakulima wamekuwa wakikabiliana nayo mara kwa mara kuwa Ni wadudu waharibifu kwenye mazao,hali ya hewa,pamoja na wizi wa mazao.
Mwishooooo
No comments